Nigeria : Watu 40 wanahofiwa kufariki katika ajali ya boti
Nairobi – Watu 40 wanahofiwa kupoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wanasafiria, kuzama katika jimbo la Kebbi, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.
Imechapishwa:
Cheza - 00:54
Maafisa wa serikali wanasema wanaendelea na msako wa kuwatafuta watu hao, lakini hawana matumaini iwapo abiria hao watapatikana wakiwa hai.
Bala Mohammed, Mkuu wa Wilaya ya Yauri amesema, msako huo ni mgumu kwa sababu ya kiwango kikubwa kwenye mto Niger, kilichochangiwa pia na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.
Ajali za boti hutokea sana nchini Nigeria kwa sababu ya kusafirisha abiria kupita kiasi, mafuriko na kutofanyika kwa ukarabati wa boti.
Mwezi uliopita, watu wengine 24 waliouawa na wengine zaidi ya 50 kutoweka wakati wakulima zaidi ya 100 walipokuwa wanasafiri katika mto Niger, wakati boti yao ilipozama.
Watu wengine 10 waliuawa, wakati boti iliyokuwa inasafirisha wafanyabiashara pia kuzama, katika jimbo la Adamawa mwezi Septemba.