Pata taarifa kuu

Nigeria: Idadi isiyojulikana ya wanafunzi wa kike wametekwa jimboni Zamfara

Nairobi – Idadi isiyojulikana ya wanafunzi wa kike wametekewa na watu wenye silaha kutoka katika chuo kikuu kimoja katika jimbo la Zamfara, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.

Wanafunzi hao walitekewa kutoka katika makaazi yao mapema siku ya Ijumaa
Wanafunzi hao walitekewa kutoka katika makaazi yao mapema siku ya Ijumaa © dailypost
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi hao walitekewa kutoka katika makaazi yao mapema siku ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa wanahabari wa ndani, watu wenye silaha waliaanza kufyatua risasi kabla ya kushambulia makaazi ya wanafunzi hao.

Hadi tukichapisha taarifa hii, maofisa wa polisi kwenye eneo hilo wala usimamizi wa chuo hicho, hawakuwa wametoa taarifa kuhusu tukio hili.

Mwaka wa 2021, watu wenye silaha waliwateka zaidi ya wanafunzi 300 wa kike kutoka katika eneo hilo la Zamfara kabla ya kuwaachia baadae baada ya mazungumzo kati ya serikali na watekaji.

Matukio ya utekekaji yamekuwa yakiripotiwa kuongezeka kaskazini Magharibi mwa Nigeria, watu wenye silaha wakiwateka raia kutoka kwenye vijiji, barabara kuu na mashambani wakitaka kulipwa kabala ya kuwaachia huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.