Pata taarifa kuu

Nigeria: Miungano ya wafanyakazi yasitisha mgomo kwa siku 30

NAIROBI – Miungano ya wafanyakazi wa umma nchini Nigeria, imekubaliana kusitisha mgomo uliokuwa umepangwa, kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha.

Mkataba wa maelewano uliofikiwa kati ya serikali ya Nigeria na Chama cha NLC na kile cha TUC, Jumatatu, Oktoba 2, 2023.
Mkataba wa maelewano uliofikiwa kati ya serikali ya Nigeria na Chama cha NLC na kile cha TUC, Jumatatu, Oktoba 2, 2023. ©
Matangazo ya kibiashara

Miungano hiyo ya Nigeria Labour Congress NLC, na Trade Union Congress TUC, imeafikiana baada ya makubaliano na serikali kuhusu juu ya hatua za kupunguza athari za mageuzi yake ya kiuchumi.

Katika mpango huu serikali imetoa nyongeza ya naira 35,000 kwa mwezi ndani ya miezi sita kwa wafanyakaz, kusimamishwa kwa muda kwa ushuru wa dizeli na uhamishaji wa fedha za uzeeni kwa Wanigeria maskini zaidi.

Tangu rais Bola Tinubu kuingia madarakani mwezi Mei, ameweka mbinu za kufufua uchumi wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuondoa ruzuku ya mafuta na pia kuweka huru sarafu ya naira, hatua ambazo maofisa wamesema ni muhimu katika kusaidia kufufua uchumi wa Nigeria.

NLC na TUC wamekubali kufuta mgomo wa nchi nzima kwa siku 30, imesema taarifa ya pamoja ya miungano hio ya serikali.

Mwenyekiti wa muungano wa TUC, Festus Osifo amewaambia waandishi wa habari kuwa anaamini serikali itatekeleza hilo kwa nia nzuri, ili kuwaondolea raia mzigo wa kupanda kwa gharama ya maisha.

Mapendekezo hayo ya serikali pia yanajumuisha kuanzishwa kwa mabasi ya usafiri wa umma yanayotumia gesi kama njia mojawapo ya kupunguza gharama ya usafiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.