Pata taarifa kuu

Urusi inasema imezua mashambulio ya ndege zisizo na rubani ya Ukraine

Urusi inasema imezuia mashambulio mawili ya ndege ziszio na rubani za Ukraine katika mji wa Moscow.

Urusi inasema imezuia mashambulio mawili ya ndege zisizo na rubani za Ukraine
Urusi inasema imezuia mashambulio mawili ya ndege zisizo na rubani za Ukraine AP - LIBKOS
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya ulinzi ya Urusi, hakujakuwa na vifo ambavyo vimeripotiwa katika mashambulio hayo ya leo Jumatatu.

Aidha wizara hiyo imesema ndege moja isiyokuwa na  rubani ya Ukraine, iliangushwa kwa kutumia mifumo yake ya kieletroniki kabla ya kuanguka katika kijiji cha Pokrovskoye katika wilaya ya Odintsovo kusini Magharibi mwa jiji kuu.

Ndege nyengine inayodaiwa na Moscow  kuwa ya Kyvi iliangushwa katika eneo la Istra, kaskazini Magharibi mwa Moscow.

Shirika la habari la RIA Novosti limesema shughuli za usafiri katika viwanja viwili vya ndege vya kimataifa katika maeneo ya Vnukovo na Domodedovo, zilisitishwa kwa muda na kuelekezwa kwengine.

Katika kipindi cha majuma ya hivi karibuni, mashambulio mawili ya ndege zisizo na rubani yamezuiwa katika mji wa kibiashara wa Moscow, yote yakiripotiwa kusababisha uharibifu mdogo. Mwezi Mei, mashambulio ya ndege hizo yalizuia karibu na Kremlin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.