Pata taarifa kuu
USALAMA-VIKWAZO

DRC: Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya maafisa waliohusika katika vurugu

Marekani imetangaza Alhamisi mfululizo wa vikwazo dhidi ya viongozi wa makundi yenye silaha yanayoendesha harakati zao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) lakini pia maafisa wa kijeshi, wanaoshutumiwa "kuchangia kuongezeka kwa vita" katika eneo hilo.

Vikwazo hivyo vinalenga viongozi watatu wa FDLR, naibu kiongozi wa M23, afisa wa cheo cha kanali kutoka jeshi la Kongo, lakini pia Brigedia Jenerali kutoka Jeshi la Ulinzi la Rwanda, ambaye vitengo vyake "viliingia kweye ardhi ya DRC na kutoa msaada kwa M23, ambayo ina uhusiano wa muda mrefu na serikali ya Rwanda."
Vikwazo hivyo vinalenga viongozi watatu wa FDLR, naibu kiongozi wa M23, afisa wa cheo cha kanali kutoka jeshi la Kongo, lakini pia Brigedia Jenerali kutoka Jeshi la Ulinzi la Rwanda, ambaye vitengo vyake "viliingia kweye ardhi ya DRC na kutoa msaada kwa M23, ambayo ina uhusiano wa muda mrefu na serikali ya Rwanda." AFP PHOTO / Roberto SCHMIDT
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Fedha, ongezeko hilo la vurugu lilianza mwishoni mwa mwaka 2021, na baada ya kuchukuliwa kwa sehemu ya eneo la mkoa wa Kivu Kaskazini, linalopakana na Rwanda, na wanamgambo wa M23, ambao Umoja wa Mataifa unatuhumu kuungwa mkono na serikali ya Rwanda.

Vuguvugu la M23 limesababisha kushadidi mapigano na jeshi la DRC pamoja na makundi mengine yenye silaha, likiwemo kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), linaloundwa na wapiganaji wa Kihutu kutoka Rwanda waliokimbilia DRC na ambao Marekani inabaini kwamba "walishirikiana na maafisa kadhaa wa jeshi la DRC".

Vikwazo hivyo vinalenga viongozi watatu wa FDLR, naibu kiongozi wa M23, afisa wa cheo cha kanali kutoka jeshi la Kongo, lakini pia Brigedia Jenerali kutoka Jeshi la Ulinzi la Rwanda, ambaye vitengo vyake "viliingia kweye ardhi ya DRC na kutoa msaada kwa M23, ambayo ina uhusiano wa muda mrefu na serikali ya Rwanda."

Vikwazo vilivyotangazwa ni pamoja na kuzuiwa kwa mali za viongozi hao wanaolengwa zinazoshikiliwa nchini Marekani na vilevile marufuku kwa raia au taasisi yoyote ya Marekani kushirikiana au kufanya biashara na watu hao. Marufuku hiyo pia inahusu usaidizi wowote wa nyenzo, kupitia chakula, bidhaa au huduma, kwa watu wanaohusika.

Mashariki mwa DRC, iliyokumbwa na vita kwa takriban miongo mitatu, inakumbwa na ongezeko la mashambulizi dhidi ya raia yanayofanywa na makundi yenye silaha na wanamgambo, na kusababisha watu wengi kuyahama makazi yao.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) iliripoti mapema mwezi Agosti kwamba "tangu mwezi Machi 2022, zaidi ya watu milioni 3.3 wamelazimika kuyahama makazi yao katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini kutokana na ghasia za kutumia silaha, na hivyo kufanya jumla ya idadi ya watu waliokimbia makazi yao katika majimbo haya matatu kufikia milioni 5.6".

Baadhi ya watu milioni 27 - zaidi ya robo ya jumla ya wakazi wa DRC - wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na watoto milioni 2.8 wanakabiliwa na utapiamlo mkali, Tume inasema.

Baadhi ya watu milioni 27 - zaidi ya robo ya jumla ya wakazi wa DRC - wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na watoto milioni 2.8 wanakabiliwa na utapiamlo mkali, Tume inasema.

Nchi hiyo pia inakabiliwa na milipuko ya mara kwa mara ya kipindupindu, surua na Ebola hasa. Siku ya Ijumaa UNICEF ilisema kuwa wagonjwa 21,400 wa kipindupindu wameripotiwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini pekee, wakiwemo watoto 8,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.