Pata taarifa kuu

DRC: Kesi ya Salomon Kalonda kuaanza kusikilizwa Alhamisi hii

Nairobi – Kesi ya Salomon Kalonda, mshauri maalum wa kisiasa wa Moise Katumbi, itaanza kusikilizwa Alhamisi hii mbele ya mahakama ya kijeshi ya Kinshasa au Gombe.

Kalonda anatuhumiwa kuwa na mawasiliano na waasi wa wa M23 na maofisa wa Rwanda kwa nia ya kufanya mapinduzi
Kalonda anatuhumiwa kuwa na mawasiliano na waasi wa wa M23 na maofisa wa Rwanda kwa nia ya kufanya mapinduzi © FMM
Matangazo ya kibiashara

Kalonda anakabiliwa na mashtaka matatu, ambayo ni uhaini,uchochezi wa mwanajeshi kutenda kinyume na majukumu yake  na ukiukaji wa sheria ya siri ya mwanajeshi baada ya kupewa hati ya siri.

Aidha anatuhumiwa kuwa na mawasiliano na waasi wa wa M23 na maofisa wa Rwanda kwa nia ya kufanya mapinduzi.

Mwezi juni 5, mshauri wa kisheria wa kitengo cha intelejensia katika jeshi, kanali Kangoli Ngoli,aliyaibua  malalamishi matatu dhidi ya  Kalonda,yakiwemo umiliki wa silaha na zana za kivita kinyume cha sheria,na kuchochea wanajeshi kuenda kinyume na majukumu yao na hivyo kutatiza hali ya usalama.

Salamon Kalonda alikamatwa May 30 katika uwanja wa ndege wa Ndjili na baadaye kuhamishwa katika gereza la jeshi la Ndolo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.