Pata taarifa kuu

Rwanda yakanusha madai ya DRC kwamba inapanga kuwatuma wanajeshi Kivu Kaskazini

Siku moja baada ya jeshi la DRC, kudai kuwa limepata taarifa za kiintelijensia kuonesha kuwa Rwanda inapanga kutuma wanajeshi wake jimbon Kivu Kaskazini, utawala wa Kigali, umekanusha madai hayo, huku nao ukiionya Congo dhidi ya jaribio lolote la kufanya mashambulio kwenye ardhi yake.

Jeshi la DRC limesema lina taarifa kwamba Rwanda inapanga kutuma wanajeshi wake jimbon Kivu Kaskazini
Jeshi la DRC limesema lina taarifa kwamba Rwanda inapanga kutuma wanajeshi wake jimbon Kivu Kaskazini © AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa jeshi la Congo, lengo la majeshi ya Rwanda ni kuongeza uwepo wao katika ardhi ya mashariki mwa nchi hiyo, likiituhumu Rwanda kushirikiana na waasi wa M23 kutekeleza vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji.

Hata hivyo jeshi la Rwanda limekanusha madai ya DRC, likiionya nchi hiyo kutojaribu kufanya shambulio kwenye ardhi yake, Kigali ikisema utawala wa Kinshasa unatafuta sababu ya kuendeleza mzozo uliopo.

Wakati huu ripoti za wataaalamu wa UN zikithibitisha Rwanda kuwasaidia waasi wa M23, Kigali inaituhumi Serikali ya Congo kwa uchokozi na hata kuanzisha vita dhidi yake.

Uhusiano kati ya Kinshasa na Kigali umetatizika kwa zaidi yam waka mmoja, DRC ikiituhumu Rwanda kushirikiana na waasi wa M23 huku Rwanda ikiituhumu Kinshasa kushirikiana na waasi wa FDLR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.