Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Biselele, aliyeshtakiwa kwa 'uhaini' na 'ujasusi na Rwanda' aachiliwa huru nchini DRC

Aliyekuwa mshauri wa kibinafsi wa rais Félix Tshisekedi, Fortunat Biselele, aliyeshitakiwa kwa "intelijensia na Rwanda", nchi jirani inayotuhumiwa kuunga mkono kundi la waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ameachiliwa Jumanne, kingana na wakili wake akinukuliwa na shirika la habari la AFP.

Kinshasa (DRC): Fortunal Biselele, mshauri wa zamani wa rais Tshisekedi, alipowasili katika mahakama ya Gombe, Ijumaa Januari 20, 2023.
Kinshasa (DRC): Fortunal Biselele, mshauri wa zamani wa rais Tshisekedi, alipowasili katika mahakama ya Gombe, Ijumaa Januari 20, 2023. © Pascal Mulegwa / RFI
Matangazo ya kibiashara

Alipokamatwa mwezi Januari mjini Kinshasa, Bw. Biselele alizuiliwa katika gereza la Makala kabla ya kuachiliwa kwa muda Julai 22. Aliyekuwa mshauri wa kibinafsi wa rais wa Jamhuri alishtakiwa kwa 'uhaini' na 'ujasusi na Rwanda'.

"Mahakama ya Kinshasa Gombe imemwachilia huru (...) Amefutiwa kabisa makosa yote yaliyokuwa yanamkabili," mwanasheria wake, wakili Richard Bondo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kisa hicho kilizuka baada ya mahojiano yaliyotangazwa kwenye video ya mtandaoni, ambapo Bw Biselele alizungumza kuhusu uhusiano wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Rais Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame.

Uhusiano huu, ambao ulionekana kuwa wa kawaida kati ya DRC na Rwanda mwanzoni mwa mamlaka ya Bw. Tshisekedi mwaka wa 2019, sasa ni mbaya kutokana na kuibuka tena kwa Vuguvugu la Machi 23 (M23), ambalo lilikuwa ni kundi la waasi wengi wa Kitutsi walioshindwa mwaka 2013, ambao walichukua silaha tena mwishoni mwa 2021.

Tangu mwanzo, Kinshasa imeishutumu Rwanda kwa kulipa silaha kundi hili la waasi na kuwasaidia katika vita yao, jambo ambalo wataalamu wa Umoja wa Mataifa walithibitisha, ingawa Kigali inakanusha.

Uamuzi wa mahakama kwa Bw. Biselele ni "ushindi unaostahili kwa sababu kesi hiyo ilikuwa ya utatuzi wa matokeo tu na majaji hawapo kwa kuunga mkono mambo ya aina hii," amesema Bw. Bondo. Ndugu wa Bw. Biselele walishutumu kesi ya kisiasa.

Nchini DRC, maafisa kadhaa wa kisiasa au usalama wanajikuta wakishutumiwa kwa kushirikiana na adui, na wanazuiliwa katika mazingira ya wasiwasi kabla ya uchaguzi.

Uchaguzi wa urais ambao utaambatana na wa wabunge wa kitaifa na wa wakuu wa mikoa pamoja na uhaguzi a serikali za mitaa umepangwa kufanyika Desemba 20.

Miezi minne kabla ya muda uliowekwa, shirika lisilo la kiserikali la Marekani la Human Rights Watch siku ya Jumanne lilishutumu "ukandamizaji" na "tisho" dhidi ya wapinzani.

Rais Tshisekedi, aliye madarakani tangu mwezi Januari 2019, anagombea muhula wa pili wa miaka mitano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.