Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Polisi wanawazuilia watu kadhaa kwa njama ya kudhoofisha usalama

Nairobi – Maofisa wa polisi nchini Sierra Leone wamewakamata baadhi ya watu wakiwemo maofisa wa jeshi ambao majina yao hayakutajwa kwa tuhuma za kudhoofisha usalama na utulivu wa taifa.

Rais Bio alizituhumu nchi za Magharibi kwa kusababsiha mchangayiko katika taifa hilo baada ya nchi hizo kuonyesha wasiwasi wake kuhusu namna uchaguzi huo ulivyofanyika.
Rais Bio alizituhumu nchi za Magharibi kwa kusababsiha mchangayiko katika taifa hilo baada ya nchi hizo kuonyesha wasiwasi wake kuhusu namna uchaguzi huo ulivyofanyika. REUTERS - PHIL NOBLE
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, polisi imesema watu wanaozuiliwa walikuwa wanapaanga maandamano yenye ghasia kati ya Agosti 7 na 10.

Polisi imewatuhumu watu inayodai wako ndani na nje ya taifa hilo kwa kuwa na njama ya kudhoofisha usalama kwenye nchi hiyo.

Licha ya kuwepo kwa njama hiyo, polisi inasema imechukuwa udhibiti wa kila jambo na kuwataka raia wa Sierra Leone kusalia watulivu na kuendelea na majukumu yao ya kawaida.

Taifa hilo la Afrika Magharibi limekuwa likikabiliwa na hali ya wasiwasi tangu kuchaguliwa tena kwa rais Julius Maada Bio tarehe 24 ya mwezi Juni.

Tarehe 5 ya mwezi Julai, Rais Bio alizituhumu nchi za Magharibi kwa kusababsiha mchangayiko katika taifa hilo baada ya nchi hizo kuonyesha wasiwasi wake kuhusu namna uchaguzi huo ulivyofanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.