Pata taarifa kuu

Kwa nini chaguo la kijeshi linawekwa mbele na ECOWAS dhidi ya Niger?

Moja ya maamuzi muhimu ya mkutano wa kilele wa  Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (WAEMU), pamoja na vikwazo vilivyotangazwa, ni makataa ya wiki moja yaliyotolewa kwa serikali ya Niger kurejesha taasisi zilizochaguliwa nchini Niger, vinginevyo chaguzi zote ziko wazi, pamoja na kuingilia kijeshi.

Wanajeshi wa kikosi cha ECOWAS mjini Banjul Januari 2017 (Picha ya zamani), ambao waliingilia kati kijeshi wakati rais wa Gambia Yaya Jammeh alipokataa kukabidhi madaraka, mwaka 2016.
Wanajeshi wa kikosi cha ECOWAS mjini Banjul Januari 2017 (Picha ya zamani), ambao waliingilia kati kijeshi wakati rais wa Gambia Yaya Jammeh alipokataa kukabidhi madaraka, mwaka 2016. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, rais wa sasa wa ECOWAS na mwenyeji wa mkutano huo, ndiye ambaye alipaza sauti: ikiwa katika wiki moja taasisi zilizochaguliwa nchini Niger hazitarejeshwa, uingiliaji kati wa kijeshi wa ECOWAS ni mojawapo ya chaguzi zinazowezekana. Kwa uamuzi huu muhimudhidi ya utawala wa kijeshi wa Niger na si kwa Guinea, Mali na Burkina Faso, Mataifa ambayo pia yanaongozwa na na jeshi bada ya kufanya mapinduzi?

Jibu kutoka kwa mwanadiplomasia wa Ghana: “Ni suala la uaminifu. Tukiruhusu mapinduzi haya yapite, basi demokrasia itakuwa hatarini na ECOWAS itakuwa haina maana yoyote, wala kuwajibika katika majukumu yake. Afisa mwingine kutoka ECOWAS anaeleza kuwa "mara tu mkutano wa mwisho wa kilele huko Bissau ulipomalizika, wataalam walikuwa wakifanyia kazi kuhusi uundwaji wa kikosi cha kikanda. Kazi inakaribia kukamilika na tunayo njia za sera yetu. "

Huko Abuja, kulingana na vyanzo vyetu, nchi kadhaa tayari zimetangaza utayari wao wa kutoa wanajeshi ikiwa ni lazima. Mwanadiplomasia wa Nigeria anaenda mbali zaidi: "Kwa upande wetu, baadhi ya wanajeshi wetu tayari wako tayari karibu na mpaka na Niger kwa operesheni ya kijeshi inayowezekana".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.