Pata taarifa kuu

Serikali ya kijeshi yaonya ECOWAS na washirika wake kuingilia kijeshi Niger

Mikutano miwili "maalum" imeandaliwa Jumapili hii katika mji mkuu wa Nigeria kujadili hali nchini Niger. Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) na Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (WAEMU) wanakutana. Lengo lililotajwa ni kulazimisha kiongozi mpya aliyetangazwa na jeshi nchini Niger, Jenerali Tchiani, kurejesha madaraka.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu alichaguliwa kuwa rais wa ECOWAS mnamo Julai 9, 2023 huko Bissau.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu alichaguliwa kuwa rais wa ECOWAS mnamo Julai 9, 2023 huko Bissau. REUTERS - TEMILADE ADELAJA
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Cotonou, Serge Daniel

Viongozi wengi kutoka ukanda huu wanatarajiwa katika mkutano wa kilele wa Abuja. Miongoni mwao tayari wametangazwa rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara na rais wa Senegali Macky Sall… Wakuu wa nchi wa Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (WAEMU) ndio ambao watakutana mwanzoni. Kiongozi wa Niger aliyetimuliwa mamlakani ndiye rais wa sasa wa umoja huo. Niger inatarajiwa kusimamishwa kwenye uanachama wa umoja huo na kuna uwezekano wa kutangaza hatua za kushinikiza utawala wa Niamey kumwachilia Rais Mohamed Bazoum na kurejea madarakani.

Utafuata mkutano wa ECOWAS. Mahamat Déby, ambaye nchi yake si mwanachama wa ECOWAS, pia amealikwa. Chad inashiriki mpaka wa pamoja na Nigeria, lakini pia na Niger. Labda hii ni dalili ya kile kitakachokuwa kiini cha mijadala.

Bola Tinubu yuko tayari kuhakikisha jeshi linarejesha madaraka

Katika mkesha wa mkutano wa kilele wa Abuja, katika miji mikuu kadhaa ya kanda hiyo, hotuba ilikuwa wazi: Msiidhinishe mapinduzi na muonyeshe nguvu zaidi ikiwa ni lazima. Alipochukua hatamu kama mkuu wa ECOWAS wiki chache zilizopita, Rais wa Nigeria Bola Tinubu alikuwa wazi: ili kuchukua mamlaka, lazima uende kwenye uchaguzi. Mapinduzi yamepitwa na wakati.

Bola Ahmed Tinubu atakuwa sauti kuu ya mkutano huu, anasema mwandishi wetu mjini Abuja, Moïse Gomis. Ni maneno gani ya utangulizi atayatamka katika utangulizi wa mkutano huo? Je, atakuwa na jukumu la kusimamia mijadala? Au itakuwa atashinikizwa kuchukuliwa kwa maamuzi ya nguvu? Tangu kuapishwa kwake, Bola Ahmed Tinubu ameapa kukabiliana na mapinduzi ya kijeshi."

Kwa upande wake, huko Niamey, Jenerali Tchiani, kiongozi mkuu wa mapinduzi, alijibu tangazo la mkutano wa kilele wa ECOWAS. Jumamosi, kwenye televisheni ya taifa, msemaji wa utawala wa kijeshi alisoma taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Jenerali Tchiani ambapo alisema anashuku ECOWAS kwa "kuandaa mpango wa uchokozi dhidi ya Niger".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.