Pata taarifa kuu

Mapinduzi Niger: ECOWAS yachukuwa vikwazo, rais wa Chad mjini Niamey kwa upatanishi

Baada ya mkutano nchini Nigeria, wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, wametoa kauli ya mwisho kwa viongozi wa mapinduzi ya kijeshi na kuamua juu ya vikwazo vya kifedha. Mahamat Idriss Déby yuko Niamey kwa upatanishi.

Rais wa Chad Mahamat Déby amepokelewa mjini Niamey na aliyekuwa Mkuu wa zamani wa Jeshi la Niger, Jenerali Salifou Mody Jumapili hii, Julai 30, 2023.
Rais wa Chad Mahamat Déby amepokelewa mjini Niamey na aliyekuwa Mkuu wa zamani wa Jeshi la Niger, Jenerali Salifou Mody Jumapili hii, Julai 30, 2023. © Gouvernement tchadien
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa habari zetu, mkuu wa nchi ya Chad, Mahamat Idriss Déby amewasili Jumapili hii, Julai 30 mjini Niamey kwa upatanishi baada ya kukutana na rais wa Nigeria Bola Tinubu, pia rais wa sasa wa ECOWAS.

Jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi ilikutana kwa faragha mjini Abuja kuamua kuhusu hatua hizo siku nne baada ya mapinduzi dhidi ya rais Mohamed Bazoum. Mwishoni mwa mkutano huu, wakuu wa nchi wametangaza makataa ya wiki moja  kurejesha utaratibu wa kikatiba nchini Niger, anaripoti mwandishi wetu huko Abuja, Moïse Gomis. Hawajaondoa suala la "kutumia nguvu" ikiwa ni lazima. Wakati huo huo, vikwazo vimechukuliwa mara moja: kufungwa kwa mipaka kisha kufutwa kwa safari za ndege kwenda Niger, hakuna tena miamala ya kibiashara na Niger, hakuna tena miamala ya nishati na Niger, kuzuiliwa mali za Niger katika benki za nchi wanachama wa ECOWAS.

Vikwazo vya kiuchumi

ECOWAS inataka kuweka vikwazo vya kweli vya kiuchumi ili kuwashinikiza viongozi wa mapinduzi ya kijeshi. Bola Ahmed Tinubu ametoa msimamo, ambao ni kutovumilia mhusika yeyote wa mapinduzi katika kanda hiyo. Wakuu wote wa Nchi na Serikali wameunga mkono hoja hiyo. Mkutano wa wakuu wa majeshi wa ECOWAS unapaswa kufanyika haraka ili kuwasilisha haraka mpango wa utekelezaji.

Rais Mohamed Bazoum anachukuliwa na wenzake kuwa rais pekee halali. Ni matendo yake na yale ya wawakilishi wake pekee ndiyo yanatambuliwa na jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi. ECOWAS inataka kuachiliwa na kurejeshwa kwa mamlaka ya mkuu wa nchi, ambaye pia inamchukulia kama mateka, kama familia yake na wajumbe wa serikali ya Niger. Wakuu wa serikali wa ECOWAS wamebaini kwamba viongozi wa mapinduzi watawajibishwa, ikiwa kwa bahati mbaya jambo baya litamtokea Mohamed Bazoum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.