Pata taarifa kuu

Ukraine: Putin ahakikisha kwamba 'atatathmini kwa uangalifu' mipango ya amani ya Afrika

Rais wa Urusi amekuwa akizungumza tangu Alhamisi na viongozi wenzake kutoka nchi za Afrika. Baada ya kutangaza kusafirisha kwa bure tani 25,000 hadi 50,000 za nafaka kwa nchi sita za bara hilo, Vladimir Putin amesema siku ya Ijumaa kwamba Urusi "itatathmini kwa makini" mapendekezo ya Afrika kutafuta suluhu la mzozo wa kivita nchini Ukraine.

Vladimir Putin anasema 'atatathmini kwa uangalifu' mipango ya amani ya Afrika kuhusu mzozo kati ya Urusi na Ukraine.
Vladimir Putin anasema 'atatathmini kwa uangalifu' mipango ya amani ya Afrika kuhusu mzozo kati ya Urusi na Ukraine. © Alexey DANICHEV / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Hebu tuchukue kwa mfano mpango wa mfululizo wa mataifa ya Afrika kusuluhisha mgogoro wa Ukraine. Ni tatizo kubwa, hatuwezi kuacha kulichunguza", ametangaza mbele ya viongozi kutoka Afrika, wakati wa iku ya pili ya mkutano kati ya Urusi na Afrika unaofanyika huko St. Petersburg.

"Ina maana kubwa, kwa sababu hapo awali, misheni za upatanishi zilihodhiwa na nchi zinazodai kuwa zenye demokrasia  iliyoendelea. Sasa, Afrika pia iko tayari kusaidia kutatua matatizo ambayo yanaonekana nje ya eneo lake", ameongeza rais wa Urusi.

"Tunaheshimu mipango yanu na tunaitathmini kwa uangalifu," ameongeza.

Katikati ya mwezi Juni, mapendekezo ya Afrika yalikataliwa na Kyiv

Mkutano wa kilele kati ya Urusi na Afrika unakuja zaidi ya wiki moja baada ya kumalizika kwa mkataba wa nafaka uliowezesha kuagiza nafaka za Ukraine nje ya nchi kupitia Bahari Nyeusi, jambo ambalo limezua wasiwasi miongoni mwa nchi za Afrika.

Katikati ya mwezi wa Juni, wajumbe wa Afrika walienda Ukraine, kisha Urusi, kutoa upatanishi wake katika mzozo huo, bila hata hivyo kupata matokeo ya haraka.

Kyiv kisha ilikataa mapendekezo ya ujumbe wa Afrika, ikibaini kwamba haingeweza kusitisha mzozo huo bila kuhakikisha kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi. Kremlin ilikuwa imeamua kuwa mpango wa Afrika ulikuwa "mgumu sana kutekeleza", huku ikihakikisha kwamba Vladimir Putin "ameonyesha nia yake ya kuuchunguza".

Mapendekezo ya amani ya Afrika yalijumuisha "kusitisha mapigano kutoka pande zote mbili", "kutambuliwa kwa uhuru" wa nchi kama unavyosema Umoja wa Mataifa na "dhamana ya usalama" kwa pande zote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.