Pata taarifa kuu

Putin anaunga mkono bara Afrika kupewa nafasi ya kudumu G20

Nairobi – Rais wa Urusi Vladimir Putin, wakati akizungumza katika ufunguzi wa mkutano kati ya taifa lake na bara Afrika mjini St Petersburg, amesema anahitaji kuona umoja wa Afrika (AU) ukipewa nafasi ya uanachama wa kudumu katika muungano wa mataifa ya G20.

Putin amesema wanatumai  kuwa uamuzi huo utafanywa mapema Septemba
Putin amesema wanatumai  kuwa uamuzi huo utafanywa mapema Septemba AP - Valery Sharifulin
Matangazo ya kibiashara

Putin amesema wanatumai  kuwa uamuzi huo utafanywa mapema Septemba, wakati wa mkutano wa kilele wa G20 huko New Delhi.

Akizungumzia kuhusu hatua ya nchi yake  kujiondoa kwenye mkataba ulioidhinishwa na umoja wa mataifa wa kuruhusu  usafirishaji wa nafaka kutoka bandari za kusini mwa Ukraine, na hatimaye kuelekea Afrika, Putin amesema kuwa Urusi inaweza kuziba pengo hilo.

Aliongeza kuwa Urusi itatoa nafaka bila malipo kwa nchi sita za Afrika katika miezi michache ijayo.

Idadi ndogo  ya viongozi wa bara Afrika wanashiriki katika mkutano huo kuliko ilivyokuwa katika mkutano wa kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.