Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-MAENDELEO

Mkutano wa Urusi na Afrika: Moscow yaelezea matarajio yake, baadhi wanataka vitendo

Siku ya pili na ya mwisho leo Ijumaa ya mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika huko Saint Petersburg Julai 28 katika kikao kisicho kuwa cha kawaida, Moscow imeanza kuelezea mikataba mingi na matarajio yake.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na viongozi wa Afrika katika Mkutano wa pili wa Wakuu wa Urusi na Afrika huko St. Petersburg Julai 28, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na viongozi wa Afrika katika Mkutano wa pili wa Wakuu wa Urusi na Afrika huko St. Petersburg Julai 28, 2023. via REUTERS - TASS
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Moscow,

Alama yauhusiano huu ambao Urusi inataka kuongeza zaidi na bara la Afrika, uwepo wake wa kidiplomasia utaongezeka: wafanyakazi zaidi, balozi zaidi pia. Vladimir Putin hivyo ametangaza kuanza kwa shughuli "hivi karibuni" ya misheni za kidiplomasia za Urusi huko Burkina Faso na Equatorial Guinea.

Rais wa Urusi, katikati ya mzozo wa Ukraine, pia anataka kuonyesha kwamba Urusi bado na daima inaweza kudumisha safu yake katika sekta ya Ulinzi: "Ili kuimarisha uwezo wa Ulinzi wa nchi za bara hili, tunaendeleza ushirikiano katika nyanja za kijeshi na kiufundi. Urusi imehitimisha makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na kiufundi na zaidi ya mataifa 40 ya Afrika, ambapo tutatoa silaha na zana mbalimbali za kijeshi. Baadhi ya bidhaa hizi hutolewa bila malipo ili kuimarisha usalama na uhuru wa Mataifa haya. "

Isipokuwa kwamba Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, anasisitiza matarajio ya uthabiti zaidi: "Kwa sababu, bila shaka, ya athari za muktadha wa kiuchumi uliotokana na janga la Uviko-19, na labda ukosefu wa uthabiti katika uandaaji wa programu za uendeshaji, maendeleo [katika baadhi ya vipengele vya ushirikiano kati ya Urusi na Afrika] limesalia kuwa pungufu tangu mkutano wa Sochi mwaka 2019. Hasa, kuimarishwa kwa ushirikiano katika masuala ya amani na usalama na mapambano dhidi ya ugaidi kunahitaji vitendo na matamko machache. "

Rais wa Umoja wa Afrika, Azali Assoumani, kwa upande wake amesisitiza: “Amani, usalama, demokrasia, haki za binadamu... Bila shaka, tunathamini sana baadhi ya washirika wetu. Lakini tunawaomba baadhi yao wasiingilie mambo yetu ya ndani.” Azali Assoumani hakuwataja washirika hawa ambao aliwataka kutoingilia maswala yao ya ndani. Kuhusu matukio ya sasa nchini Niger, kwa vyovyote vile amebainisha: “Tunapambana dhidi ya mabadiliko yasiyo ya kikatiba, kwa sababu kinachotokea wakati mwingine katika bara letu hakitakuwa na manufaa kwa nchi zetu. Sisi, Umoja wa Afrika, tunalaani mabadiliko yasiyo ya kikatiba ambayo yametokea nchini Niger, na pia tunajiunga na jumuiya ya kimataifa katika suala hili”.

Mkutano huo na orodha yake ya matamanio na mikataba unaendelea hadi Ijumaa jioni, lakini tayari Kremlin, kupitia sauti ya msemaji wake, inaihakikisha: mkutano ujao wa Urusi na Afrika uko kwenye programu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.