Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Kiongozi wa upinzani ametupilia mbali matokeo ya awali

Nairobi – Nchini Sierra Leone, mgombea wa upinzani Samura Kamara, ametupilia mbali matokeo ya urais ya awali ambayo ameyataja kama "wizi wa mchana", akidai kuwa mawakala wake wa uchaguzi hawakuruhusiwa kuthibitisha zoezi la kuhesabu na kujumulisha kura.

Upinzani nchini Sierra Leone umetupilia mbali matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais
Upinzani nchini Sierra Leone umetupilia mbali matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais REUTERS - COOPER INVEEN
Matangazo ya kibiashara

Matamshi yake yanakuja wakati huu idadi kubwa ya kura zikiwa zimehesabiwa ambapo matokeo yanaonyesha rais wa sasa, Julius Maada Bio,  akiwa mbele ya mpinzani wake, Samura Kamara.

Haya yanajiri wakati huu waangalizi wa Umoja wa Ulaya wakiituhumu tume ya uchaguzi kwa kutokuwa na uwazi ambapo pia wameshuhudia visa vya machafuko katika baadhi ya maeneo nchini wakati wa upigaji kura.

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, anaongoza katika uchaguzi huo kwa mujibu wa matokeo ya awali
Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, anaongoza katika uchaguzi huo kwa mujibu wa matokeo ya awali REUTERS - COOPER INVEEN

Tume ya uchaguzi nchini Sierra Leone imesema inatarajia kuwachapisha matokeo kamili ya uchaguzi huo wa urais uliofanyika siku ya Jumapili baadae bila ya kuweka wazi tarehe kamili ya kufanya hivyo.

Huku 60% ya vituo vya kupigia kura vikiwa vimehesabiwa, tume ilisema kuwa Julius Maada Bio alikuwa anaongoza akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Samura Kamara wa All People's Congress (APC).

Shughuli za kuhesabu kura inaendelea nchini Sierra Leone
Shughuli za kuhesabu kura inaendelea nchini Sierra Leone REUTERS - COOPER INVEEN

Mwenyekiti wa kundi la waangalizi, Yemi Osinbajo, alisema katika taarifa kwamba uchaguzi umekuwa "wa amani kwa kiasi kikubwa". Hata hivyo, kulikuwa na ripoti za changamoto za vifaa ambazo zilisababisha kucheleweshwa kwa siku ya uchaguzi, alisema.

"Tulifurahishwa na kujitokeza kwa wapiga kura kwa kiasi kikubwa na uendeshaji wa amani wa zoezi hilo  kwa kiasi kikubwa." alisema Yemi Osinbajo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.