Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Takriban watu 16 wauawa katika mashambulizi mawili mapya katikati mwa Nigeria

Takriban watu 16 wameuawa katika jimbo la Plateau katikati mwa Nigeria, eneo linalokumbwa na mapigano makali kati ya wakulima na wafugaji, jeshi limesema leo Alhamisi.

Msururu wa mauaji yanayofuatiwa na ulipizaji kisasi na kutokuwepo kwa haki madhubuti kumesababisha kuibuka kwa uhalifu mkubwa katika eneo hilo na magenge ambayo yanaongoza msafara katika vijiji, ambapo wanaua wakazi kwa makumi na kufanya utekaji nyara ili kuwakomboa kwa fidia.
Msururu wa mauaji yanayofuatiwa na ulipizaji kisasi na kutokuwepo kwa haki madhubuti kumesababisha kuibuka kwa uhalifu mkubwa katika eneo hilo na magenge ambayo yanaongoza msafara katika vijiji, ambapo wanaua wakazi kwa makumi na kufanya utekaji nyara ili kuwakomboa kwa fidia. AP - APTN
Matangazo ya kibiashara

Kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria mara kwa mara ni eneo la mivutano na mizozo mibaya kuhusiana na ardhi na rasilimali za maji kati ya jamii za wakulima na wafugaji.

Katika ghasia za hivi punde siku ya Jumanne, watu sita kutoka kundi la wakulima la kujilinda waliuawa na watu wenye silaha katika wilaya ya Riyom, wakati wengine kumi waliuawa katika shambulio katika mkoa wa Mangu, msemaji wa jeshi amesema.

"Watu sita waliuawa huko Riyom," Meja Ishaku Takwa aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano. "Shambulio lingine lilifanyika katika baadhi ya jamii za Wamangu na watu 10 waliuawa."

Bala Fwangje, mbunge wa eneo la Mangu Kusini, amesema watu 14 wameuawa katika eneo hilo. "Tumegundua kuwa watu 14 wameuawa, nyumba zimeharibiwa na mali kuchomwa. Bado sijapata maelezo yote," Fwangje amesema.

Tangu mwezi Mei, ghasia zimeua zaidi ya watu 200 kati ya jamii za wakulima wa Berom na jamii za wafugaji wa Fulani katika mikoa ya Riyom, Barkin Ladi na Mangu.

Msururu wa mauaji yanayofuatiwa na ulipizaji kisasi na kutokuwepo kwa haki madhubuti kumesababisha kuibuka kwa uhalifu mkubwa katika eneo hilo na magenge ambayo yanaongoza msafara katika vijiji, ambapo wanaua wakazi kwa makumi na kufanya utekaji nyara ili kuwakomboa kwa fidia.

Dhuluma hizi ni mojawapo ya changamoto nyingi za kiusalama zinazomkabili Rais Bola Tinubu mkuu wa nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika, na yenye uchumi mkubwa zaidi barani humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.