Pata taarifa kuu

Nigeria: Serikali ya Kano yatangaza hali ya dharura kukabiliana na uhalifu

NAIROBI – Maofisa katika jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria, wametangaza hali ya dharura kutokana na wizi wa simu pamoja na visa vingine vya uhalifu katika mji wa Kano, vyombo ya habari vya ndani vimeripoti.

Abiria akiwa amebebwa kwenye pikipiki katika jimbo la Kano akiwa na kisu wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita.
Abiria akiwa amebebwa kwenye pikipiki katika jimbo la Kano akiwa na kisu wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita. AP - Sani Maikatanga
Matangazo ya kibiashara

Bunge limeeleza kuguswa na ongezeko la wizi wa simu, vitendo vya wizi kwenye maduka, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na matukio mengine ya kihalifu yanayotishia usalama wa mji huo.

Wakati wa majadiliano ya muswada kuhusu masuala hayo uliowasilishwa na kiongozi wa wengi bungeni, wabunge walikubaliana kwamba kuna umuhimu wa kutatua changamoto hiyo kabla ya hali kuwa mbaya Zaidi.

Bunge limeudhinisha muswada huo na kutoa wito kwa serikali ya jimbo hilo kuhakikisha wanaohusika na vitendo vya kihalifu wanakabiliwa na mkono wa sharia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.