Pata taarifa kuu

Watu 20 wameuawa kwenye vurugu katika jimbo la plateau nchini Nigeria

NAIROBI – Takriban watu 20 wameuawa katika vurugu za hivi punde kati ya jamii za wafugaji na wakulima katika jimbo la Plateau nchini Nigeria, kwa mujibu wa polisi.

Ramani ya Nigeria
Ramani ya Nigeria AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa polisi wa jimbo la Plateau, Alfred Alabo ameiambia AFP, kuwa shambulio hili la hivi punde, limetokea baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji kuvamia jamii ya wakulima siku ya Jumapili, katika wilaya ya Barkin Ladi.

Mara kwa mara jimbo hilo limekuwa likishuhudia ongezeko la mivutano ya kijamii kati ya wafugaji Waislamu wa Fulani na jamii nyingi za wakulima wa Kikristo, kuhusu ardhi na maji hasa katika wilaya za Mangu, Barkin Ladi na Riyom.

Gavana wa eneo hilo Caleb Manasseh Mutfwang, amelaani vikali tukio, akiitaka idara ya usalama kushughulikia hili ili kukomesha umwagaji damu na uharibifu wa mali.

Tangu katikati ya mwezi Mei mwaka huu, takriban watu 140 wameuawa katika mvutano wa kijamii huko Plateau huku zaidi ya watu elfu tatu wakikimbia makazi yao.

Mvutano huu kati ya wafugaji na wakulima, umechochea zaidi uhalifu, huku magenge yenye silaha nzito yakilenga vijiji kwa utekaji nyara mkubwa, uporaji na mauaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.