Pata taarifa kuu

Nigeria: Rais Tinubu amewafuta kazi maofisa wakuu wa usalama

NAIROBI – Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu amewafuta wakuu wa usalama wa nchi hiyo na wakuu wa polisi katika mabadiliko makubwa ambayo ameyatekeleza.

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu REUTERS - TEMILADE ADELAJA
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa ulinzi, mkuu wa jeshi, jeshi la wanamaji na jeshi la wanahewa wote wamesimamishwa kazi, nyadhifa zao zikichukuliwa na maofisa wengine.  

Tinubu pia amevunja bodi za taasisi zote za serikali ya shirikisho isipokuwa ile ya baraza la mahakama, baraza la uchaguzi na tume ya huduma ya polisi.

Mabadiliko hayo ya usalama yanajiri wiki mbili baada ya kukutana na wakuu wa usalama na kuwataka kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto za ugaidi, uasi, ujambazi, wizi wa mafuta na uharamia.

Nigeria imekuwa ikikabiliwa na wimbi la mashambulio yanayotekelezwa na  makundi ya wanajihadi na magenge mengine ya wahalifu, wakiwemo majambazi ambao hujihusisha zaidi na utekaji nyara ili kujipatia fidia.

Kumekuwepo na wito wa mara kwa mara kutoka kwa mashirika ya kiraia wakati wa serikali iliyopita kutaka wakuu wa usalama wabadilishwe kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.