Pata taarifa kuu

Sudan: G7 yataka mapigano kukomeshwa 'mara moja'

Mawaziri wa mambo ya nje wa G7 Jumanne tarehe 18 Aprili walitoa wito wa kukomeshwa 'mara moja' kwa mapigano nchini Sudan. Tangu Jumamosi, mapigano kati ya jeshi la serikali linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah Al-Bourhane na vikosi vya kijeshi vya mshirika wake wa zamani, Jenerali Mohammed Hamdan Daglo, anayejulikana kama "Hemetti", yamesababisha karibu watu 200 kuuawa na takriban 1,800 kujeruhiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Wanadiplomasia kutoka kundi la nchi zilizoendelea kiviwanda, G7, wakitaka mapigano kukomeshwa mara moja.
Wanadiplomasia kutoka kundi la nchi zilizoendelea kiviwanda, G7, wakitaka mapigano kukomeshwa mara moja. © Мелані Жолі / Twitter
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali hii, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa majenerali hao wawili "kukomesha mara moja uhasama" kwa sababu unaweza "kuwa mbaya kwa nchi na kanda nzima". Lakini mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, amesema hana matumaini makubwa kuhusu kurejea kwa haraka kwa mazungumzo wakati "ni vigumu kutathmini ni upande gani uwiano unabadilika".

"Tunazitaka pande zote kukomesha ghasia mara moja, kupunguza mvutano na kurejesha utawala wa kiraia nchini Sudan," mawaziri wa mambo ya nje wa nchi kubwa zilizoendelea kiviwanda wamesema baada ya kukutana nchini Japan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kwa upande wake, alizungumza kando siku ya Jumanne na majenerali hao wawili hasimu wanaopigania mamlaka nchini Sudan na kusisitiza "udharura wa kufikiwa kwa usitishaji mapigano", kulingana na msemaji wake, Vedant Patel.

Kusitishwa kwa mapigano "kutasaidia kutoa misaada ya kibinadamu kwa wale walioathiriwa na mapigano, kuunganisha familia za Sudan [zilizotawanywa na mapigano] na kuhakikisha usalama wa wanachama wa jumuiya ya kimataifa huko Khartoum", kulingana na kauli ya Bw. Blinken iliyonukuliwa na na Bw. Patel katika taarifa.

Siku ya Jumatatu, msafara wa kidiplomasia wa Marekani kuelekea Sudan ulishambuliwa, lakini hakuna aliyejeruhiwa. Antony Blinken alikiita kitendo cha "kutowajibika". Siku hiyo hiyo, balozi wa Umoja wa Ulaya nchini humo alishambuliwa nyumbani kwake.

Mapigano hayo yalizuka baada ya wiki kadhaa za myukano wa kuwania madaraka kati ya majenerali wawili walionyakua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2021. Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, na makamu wake, Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza Kikosi chenye nguvu cha Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF).

Umoja wa Mataifa umesitisha shughuli zake nyingi nchini humo, alisema msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric, ambaye alisisitiza Umoja wa Mataifa hautakuwa na ulazima wa kuwahoji wahudumu wake wasipotokea maofisini kutokana na mashaka ya usalama.

wakazi wa Sudan wakabiliwa na hali mbaya ya maisha

Katika taarifa yake, mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths amesema mapigano hayo mapya yanazidisha hali ambayo tayari ilikuwa tete, na kulazimisha mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika weo katika huduma za kiutu  kufunga kwa muda programu zao zote zaidi ya 250 kote Sudan.

Aliongeza kwa kusema athari za kusimamishwa huko zitaonekana mara moja, haswa katika maeneo ya ambayo hali ya uhakika wa chakula na msaada wa lishe imekuwa duni, katika nchi ambayo watoto milioni 4 na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wapo katika mazingira magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.