Pata taarifa kuu

Msafara wa wanadiplomasia wa Marekani washambuliwa Sudan

Msafara wa wanadiplomasia wa Marekani nchini Sudan umelengwa na mashambulizi siku ya Jumatatu, Aprili 17, lakini hakuna aliyejeruhiwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema leo Jumanne, akitaja kitendo 'cha aibu na kisichokubalika', shirika la habari la AFP limeripoti.

Zaidi ya watu 180 wameuawa na wengine 1,800 kujeruhiwa katika mapigano ya silaha kati ya mahasimu wa kijeshi nchini Sudan tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, alitangaza, mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Aprili 17, 2023.
Zaidi ya watu 180 wameuawa na wengine 1,800 kujeruhiwa katika mapigano ya silaha kati ya mahasimu wa kijeshi nchini Sudan tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, alitangaza, mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Aprili 17, 2023. © Servet Gunerigok
Matangazo ya kibiashara

Sudan bado inakumbwa na vita vya viongozi kati ya majenerali wawili wenye nguvu wanaowania madaraka katika nchi hii.

Idadi ya watu waliouawa imeongezeka huku takriban watu 200 wakiuawa miongoni mwa raia.

Sudan inaendelea kukumbwa na mapigano makali yanayochochewa na viongozi wawaili wanaowania madaraka. Tangu Jumamosi, Aprili 15, nchi hii imekumbwa na vita vya viongozi kati ya wanajeshi wawili wenye nguvu: Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, kiongozi mkuu wa nchi hiyo, na nambari wake wa pili, Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana kama "Hemedti" , mkuu wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (FSR), ambacho kwa pamoja kiliwaondoa raia madarakani wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Oktoba 2021.

Karibu watu 200 wauawa na 1,800 kujeruhiwa

Baada ya siku tatu za mapigano, siku ya Jumatatu, mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Josep Borell, alitangaza kwamba balozi wa Umoja wa Ulaya "ameshambuliwa" nyumbani, na kukemea "ukiukaji wa wazi" wa Mkataba wa Vienna na kukumbusha kuwa mamlaka ya Sudan inawajibika katika kuhakikisha usalama wa balozi mbalimbali za nchi za kigeni katika nchi yao. Siku hiyo hiyo, msafara wa wanadiplomasia wa Marekani uliponea baada ya kushhambuliwa na wapiganaji, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Jumanne, na kuongeza kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa na kulaani kitendo 'kiovu'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.