Pata taarifa kuu

Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa 'kukomeshwa mara moja kwa uhasama' nchini Sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa majenerali wawili wanaogombania madaraka nchini Sudan "kusimamisha mara moja uhasama" katika siku ya tatu ya mapigano makali.

Katiu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Katiu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. AP - Achmad Ibrahim
Matangazo ya kibiashara

"Ninalaani vikali kuzuka kwa mapigano yanayotokea Sudan na kutoa wito kwa viongozi wa vikosi vya majeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka kusitisha mara moja uhasama, kurejesha utulivu na kuanza mazungumzo ya kutatua mgogoro," amesema. .

Mzozo huo ulikuwa umefichwa kwa wiki kadhaa kati ya mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, kiongozi mkuu wa nchi, na naibu wake, Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana kama "Hemedti", mkuu wa Vikosi vya msaada wa haraka (FSR), ambao kwa pamoja waliwaondoa raia mamlakani wakati mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Oktoba 2021.

Tangu Jumamosi, mapigano ya silaha nzito hayajakoma na jeshi la anga linalenga mara kwa mara, hata katikati ya Khartoum, makao makuu ya FSR, wanamgambo wa zamani kutoka vita katika eneo la Darfur ambao wamekuwa wasaidizi rasmi wa jeshi. Takriban raia 100 wameuawa, kwa mujibu wa chama rasmi cha madaktari.

"Ongezeko lolote zaidi linaweza kuwa mbaya kwa nchi na kanda nzima," ameonya Antonio Guterres, akiwatolea wito "wale wote ambao wana ushawishi katika hali hiyo kuitumia kwa amani". "Hali ya kibinadamu nchini Sudan tayari ni ya wasiwasi, sasa ni janga," ameongeza.

Wakati maafisa watatu wa shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, waliuawa, pia amerudia wito wake kwa wahusika "kuhakikisha usalama" wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wote wa mashirika ya kutoa misaada. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo pia lillitaka kusitishwa kwa mapigano siku ya Jumapili, linatazamiwa kujadili hali hiyo siku ya Jumatatu katika mkutano wa faragha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.