Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Polisi yapinga ripoti ya Amnesty

Polisi ya Sierra Leone imepinga ripoti ya shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International lililoshutumu "matumizi ya nguvu kupita kiasi" wakati wa ghasia mbaya za mwezi Agosti 2022.

Wakazi wa moja ya mitaa ya Freetown waandamana kupinga dhidi ya gharama kubwa ya maisha na serikali, Agosti 10, 2022.
Wakazi wa moja ya mitaa ya Freetown waandamana kupinga dhidi ya gharama kubwa ya maisha na serikali, Agosti 10, 2022. REUTERS - UMARU FOFANA
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa maandamano haya ya kupinga gharama kubwa ya maisha ambayo iligeuka kuwa ghasia, maafisa sita wa polisi na raia 27 waliuawa kulingana na ripoti rasmi kutoka nchi hii ndogo ya Afrika Magharibi. Matumizi ya nguvu yalikuwa "ya sawia, yenye busara na ya lazima", polisi imesema katika taarifa. Polisi pia imelikosoa shirika la Amnesty kwa kutozingatia "unyama" ambapo baadhi ya maafisa wa polisi waliuawa siku hiyo.

Ili kutoa ripoti hii iliyochapishwa Jumatatu, Amnesty International inasema ilizungumza na mashahidi, ndugu na rafiki wa waathiriwa, maafisa, polisi na mashirika ya kiraia. Kwa mfano, ilikusanya ushuhuda wa baba ambaye binti yake mwenye umri wa miaka 22 "alipigwa risasi" na vikosi vya usalama, wakati "alipokuwa akienda kuuza mboga" na hakushiriki katika maandamano.

Polisi iliwakamata wakati wa fujo hizi "watu 515", waliofunguliwa mashitaka hasa kwa "uharibifu wa makusudi wa mali, tabia ya uchochezi na mauaji", lakini idadi ambayo bado iko kizuizini "haijafichuliwa", kulingana na Amnesty.

Wakati wa maandamano yenye vurugu, vikosi vya usalama "vinapaswa kutumia nguvu tu wakati vitakuwa vimetumia njia nyingine zote za amani zikashindikana," Amnesty imeongeza. Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, aliyechaguliwa mwaka 2018 na kuwania muhula wa pili, amesema ghasia hizo zililenga kuunda "uasi" wa kupindua serikali na akalaumu upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.