Pata taarifa kuu
HAKI-MAWASILIANO

Amnesty International yalaani kuzuiwa kwa mitandao kadhaa ya kijamii nchini Ethiopia

Shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International siku ya Alhamisi limetoa wito kwa mamlaka ya Ethiopia kuondoa kizuizi cha ufikiaji wa mitandao kadhaa ya kijamii, ikiwa ni pamoja na Facebook, Telegram, TikTok na Youtube, ambavyo havijafikiwa tangu Februari 9 nchini Ethiopia.

Mamlaka za Ethiopia zimekata mara kwa mara au kuzuia ufikiaji wa mtandao au baadhi ya majukwaa katika miaka ya hivi karibuni.
Mamlaka za Ethiopia zimekata mara kwa mara au kuzuia ufikiaji wa mtandao au baadhi ya majukwaa katika miaka ya hivi karibuni. 路透社
Matangazo ya kibiashara

"Mamlaka ya Ethiopia, kwa muda wa mwezi mmoja uliopita, imekuwa ikiwazuia watu nchini humo kuingia kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii", hatua ambayo "inakiuka kwa uwazi haki za raia za uhuru wa kujieleza na kupata habari", ameshutumu katika taarifa kwa vyombo vya habari Naibu mkurugenzi wa Amnesty International katika ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Flavia Mwangovya.

Kurasa za wavuti za Facebook, Telegram, TikTok na Youtube au appli zao za simu bado hazijapatikana siku ya Alhamisi nchini Ethiopia, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wamebaini. Shirika la Open Observatory of Network Interference (OONI), chama cha kuchunguza udhibiti, limebaini kwamba mitandao hii ya kijamii inazuiwa tangu Februari 9.

Kulingana na Amnesty International, vizuizi hivi ni mfululizo wa wito wa maandamano yaliyoanzishwa na viongozi wa Kanisa la Orthodox la Ethiopia nchini humo kupinga kuundwa kwa kundi la upinzani hivi karibuni.

Abune Mathias, patriarki wa Kanisa la Tewadeho, ambalo linaleta pamoja takriban 40% ya wakazi takriban milioni 120, amemkosoa Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwa kutoa aina ya utambuzi kwa "kundi haramu" lililotengwa na amemshutumu kwa " kuingilia kati katika masuala ya kidini”.

Maandamano hayo hatimaye yalisitishwa baada ya mkutano kati ya viongozi wa Kanisa na Bw. Abiy. 

Mamlaka za Ethiopia zimekata mara kwa mara au kuzuia ufikiaji wa mtandao au baadhi ya majukwaa katika miaka ya hivi karibuni. Serikali iliyopita ilifanya hivyo mara kadhaa kati ya 2015 na 2017, wakati ilikabiliwa na vuguvugu la maandamano ambalo halijalinganishwa kwa miaka 25. Hii pia imekuwa kesi tangu Bw Abiy aingie mamlakani mwaka wa 2018.

Eneo la kaskazini la Tigray, eneo la mgogoro wa silaha na serikali ya shirikisho, kwa kiasi kikubwa lilinyimwa njia yoyote ya mawasiliano ya simu kwa miaka miwili. Mitandao imerejeshwa kwa kiasi tangu kusainiwa kwa makubaliano ya amani mnamo mwezi Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.