Pata taarifa kuu
ETHIOPIA- USALAMA

Ethiopia: Watu 50 wameuawa katika uvamizi wa kikabila

NAIROBI – Tume ya haki za binadamu nchini Ethiopia inasema watu 50 wameuawa mwezi huu katika jimbo la Oromia, kufuatia uvamizi wa kikabila.

Tume ya haki za binadamu nchini Ethiopia inasema watu 50 wameuawa mwezi huu katika jimbo la Oromia, kufuatia uvamizi wa kikabila.
Tume ya haki za binadamu nchini Ethiopia inasema watu 50 wameuawa mwezi huu katika jimbo la Oromia, kufuatia uvamizi wa kikabila. RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake, Tume hiyo inasema tarehe mbili ya mwezi huu, watu waliokuwa wamejihami kwa bastola, walivamia mji wa Ano, unaowahifadhi wakimbizi wa ndani zaidi ya Elfu 10 na kuanza kuwauwa, nyumba baada ya nyumba.

Inaelezwa kuwa watu hao wenye silaha, baada ya kuvamia kambi hiyo, waliwazingira wanaume ambao walishindwa kutoroka huku baadhi yao miili yao ikiteketezwa moto baada ya kuuawa, huku watu waliolengwa wakiwa kutoka kabila la Amhara.

Waliotekeleza mauaji hayo walionekana wamevalia sare za kundi la wapiganaji la Oromo Liberation Army (OLA), na mauaji haya yamejiri baada ya utulivu kuanza kushuhudiwa jimboni Tigray.

Hata hivyo, mapigano yameendelea jimboni Oromia, ambao ndio wengi nchini Ethiopia, na ambao kwa miaka mingi wameendelea kulalamikia kutengwa na serikali jijini Addis Ababa, lakini wapiganaji wake wanakanusha kuhusika na mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.