Pata taarifa kuu

Ethiopia: Viongozi wa TPLF wakanusha kuunda serikali ya mpito

NAIROBI – Nchini Ethiopia, viongozi wa kundi la waasi la Tigray, wamekanusha ripoti kuwa wameunda serikali ya mpito katika jimbo hilo la Kaskazini, baada ya mkataba wa amani na serikali ya Addis Ababa mwaka uliopita.

Wapiganaji wa TPLF na serikali ya Ethiopia mwaka jana walikubaliana kusitisha mapigano
Wapiganaji wa TPLF na serikali ya Ethiopia mwaka jana walikubaliana kusitisha mapigano AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa kundi hilo Getachew Reda amekanusha ripoti hizo na kusema utawala wa mpito wa Tigray utaanzishwa baada ya mashauriano ya pande zote kwa mujibu wa mkataba wa amani.

Kwa mujibu wa mkataba wa amani ulioleta amani katika jimbo hilo baada ya mapigano ya miaka miwili, serikali itakayoundwa inapaswa kuidhinishwa na serikali ya Shirikisho jijini Addis Ababa.

Baada ya kurejea kwa amani, vyama vya siasa kutoka upinzani katika êneo hilo, vimekuwa vikishininikiza serikali ya pamoja ya mpito ili wadau wote wa siasa washirikishwe katika uongozi wa Tigray.

Mwezi uliopita, vyama vya hivyo vya siasa vilisusia mkutano wa kuundwa kwa serikali ya mpito, vikishutumu kuwepo kwa mpango wa kudhofisha mchakato wa kuundwa kwa serikali ya pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.