Pata taarifa kuu

Ethiopia: Uchunguzi wa UN Tigray unaweza 'kudhoofisha' makubaliano ya amani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia alionya Jumatano kwamba uchunguzi unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kutoa mwanga kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu huko Tigray unaweza 'kudhoofisha' maendeleo kwenye mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka jana.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Demeke Mekonnen mnamo Septemba 25, 2021 katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Demeke Mekonnen mnamo Septemba 25, 2021 katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. AP - Kena Betancur
Matangazo ya kibiashara

Vita viliharibu Tigray kwa miaka miwili. Makubaliano ya amani yalitiwa saini Novemba 2022 huko Pretoria, Afrika Kusini, kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa eneo hili la kaskazini mwa Ethiopia.

Katika ripoti iliyochapishwa mwezi Septemba 2022, wataalam huru wa Umoja wa Mataifa 'walishuku uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu huko Tigray', uliofanywa na pande zote.

Serikali ya Ethiopia, huku ikiikataa ripoti hiyo, imeanza mashambulizi ya kidiplomasia ili kuwazuia wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuendelea na kazi yao.

Siku ya Jumatano, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje Demeke Mekonnen aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba uchunguzi huo 'unaweza kudhoofisha mchakato wa amani unaoongozwa na Umoja wa Afrika na utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Pretoria'.

Katika mkutano na waandishi wa habari wiki jana, Rais wa Eritrea Issaias Afeworki alipuuzilia mbali shutuma za ukiukwaji wa haki za binadamu unoadaiwa kutekelezwa na jeshi lake huko Tigray, na kuita madai hayo kuwa na 'potofu'.

Wanajeshi wa Eritrea waliunga mkono vikosi vya serikali ya Ethiopia katika mashambulizi yao yaliyoanzishwa mwezi Novemba 2020 dhidi ya vikosi vya mamlaka ya waasi katika eneo la Tigray. Marekani na mashirika ya kutetea haki za binadamu yalishutumu wanajeshi wa Eritrea kwa kufanya ukatili wakati wa mzozo huo, ikiwa ni pamoja na mauaji ya mamia ya raia.

Addis Ababa na Asmara kwa miezi kadhaa wamekana Eritrea kuhusika na kitendo chochote katika jimbo la Tigray. Mwishoni mwa mwezi Machi 2021, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed hatimaye alikubali uwepo wao. Kuondoka kwao kulitangazwa mara kadhaa, lakini kamwe hakuthibitishwa. Wanajeshi hawa wameshutumiwa kwa uporaji, mauaji na ubakaji wakati wote wa mzozo huo, hasa katika jiji la Aksoum au kijiji cha Dengolat.

Asmara hakushiriki katika mijadala ya makubaliano ya amani, ambayo yalitoa mpango wa kupokonya silaha kwa vikosi vya Tigraya, ambao ulitakiwa kufanywa kwa "wakati mmoja na kuondoka kwa vikosi vya kigeni nchini Ethiopia", ikimaanisha Eritrea, ambayo haikutajwa kamwe kwenye nakala hiyo. Waasi wa Tigraya walianza kusalimisha silaha zao nzito tangu mwezi wa Januari.

Mjumbe wa Umoja wa Afrika katika Pembe ya Afrika, Olusegun Obasanjo, alisema katikati ya mwezi wa Januari kwamba hadi watu 600,000 waliaminika kuuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.