Pata taarifa kuu
UCAGUZI-SIASA

Chama tawala chapata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa wabunge Djibouti

Chama tawala nchini Djibouti, nchi ndogo katika Pembe ya Afrika, kwa  mshangao mkubwa kimeshinda uchaguzi wa wabunge wa siku ya Ijumaa, mshauri wa rais ameliambia shirika la habari la AFP leo Jumanne, siku chache baada ya kutangazwa kwa matokeo ya awali.

Wafuasi wa Rais wa Djibouti Ismael Omar Guelleh wakiandamana bungeni Aprili 19, 2010.
Wafuasi wa Rais wa Djibouti Ismael Omar Guelleh wakiandamana bungeni Aprili 19, 2010. AFP/Simon MAINA
Matangazo ya kibiashara

Vyama vikuu vya upinzani vilisusia uchaguzi huu uliolenga kuwateua wabung 65 wa Baraza la Wawakilishi, ambalo tayari limetawaliwa kwa muda mrefu na Muungano wa Walio Wengi wa rais (UMP), chama cha Rais Ismael Omar Guelleh, madarakani tangu 1999.

UMP ndicho chama pekee kilichojiwasilisha katika maeneo sita ya nchi hii yenye takriban wakazi milioni moja. Chama cha UMP kilipambana na chama cha UDJ, kilishindwa katika majimbo mawili pekee. UMP ilichukua viti 58 katika Bunge lililomaliza muda wake, dhidi ya 5 vya UDJ.

"Kutokana na kutokuwepo kwa changamoto yoyote kwa upande wa vyama viwili, Baraza la Katiba linaweza tu kuthibitisha matokeo ya muda, yaani: viti 58 vya UMP na 7 vya UDJ", alitangaza Alexis Mohamed, mshauri maalum wa Rais. Waziri wa Mambo ya Ndani alitangaza matokeo haya ya awali siku ya Jumamosi.

"Ushindi huu ni wa matumaini katika kukabiliana na hali ya kukata tamaa, ya umoja na mshikamano mbele ya chuki na migawanyiko. Ushindi huu ni wa Djibouti na Wadjibouti," alisema stride Waziri Mkuu Abdoulkader Kamil Mohamed siku ya Jumamosi.

Alexis Mohamed alifafanua kuwa UDJ walizingatia kwa muda kupinga baadhi ya matokeo haya, kabla ya kubadilisha mawazo yao. "Baraza la Katiba lina siku 15 kuthibitisha au kubatilisha matokeo. Hata hivyo, hili linaweza kufanyika vizuri kabla ya muda mrefu kama hakuna mgogoro wa pande zote mbili", ameongeza mshauri huyo wa rais.

Djibouti, koloni la zamani la Ufaransa hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1977, ni jimbo tulivu lililo katikati ya eneo lenye matatizo na ambalo linaamsha shauku ya madola makubwa. Inapokea hasa kambi za kijeshi za Amerika, Ufaransa na China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.