Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Waasi wa FRUD waachilia wanajeshi 6 wa Djibouti waliokuwa wakizuiliwa tangu mwezi Oktoba

Wanajeshi sita wa Djibouti waliokuwa wakizuiliwa na kundi la waasi tangu shambulio la kambi yao Oktoba 7 wameachiliwa, waasi na serikali ya Ethiopia, ambayo ilishiriki katika mazungumzo hayo, walitangaza siku ya Jumatano.

Moja ya mitaa ya Djibouti (picha ya kumbukumbu).
Moja ya mitaa ya Djibouti (picha ya kumbukumbu). © Wikimedia Creative Commons/CC BY 3.0
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi saba wa Djibouti waliuawa na wengine sita kutoweka wakati wa shambulio dhidi ya kambi ya Garabtisan, kaskazini mwa nchi hii ndogo katika Pembe ya Afrika.

Wizara ya Ulinzi ya Djibouti kisha ikanyooshea kidole "Armed FRUD" (kundi la waasi, ikiielezea kama "kundi la kigaidi".

"Hatutaki kwa njia yoyote kuendeleza mateso na wasiwasi wa familia za askari waliokuwa wakifungwa, tumechukua uamuzi wa kuwakabidhi askari walioangukia mikononi mwetu kwa viongozi wa Ethiopia”, FRUD ilisema katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, nchi jirani ambayo ilishiriki katika mazungumzo ya kuachiliwa kwa wanajeshi hao, imethibitisha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba wanajeshi hao "wamekabidhiwa kwa serikali ya Djibouti", na kusisitiza kuwa nchi hizo mbili zinshirikiana ili kuimarisha ushirikiano katika masuala ya amani na usalama".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.