Pata taarifa kuu

Wanajeshi saba wauawa katika shambulizi kwenye kambi yao nchini Djibouti

Wizara ya Ulinzi imelinyooshea kidole cha lawama kundi la  Front for the Restoration of Unity and Democracy kuhusika na shambulio lililogharimbu maisha ya wanajeshi saba, likilielezea kama "kundi la kigaidi".

Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh mjini Addis Ababa mwaka 2014.
Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh mjini Addis Ababa mwaka 2014. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi saba wa Djibouti waliuawa katika shambulio kwenye kambi yao na kundi la waasi mapema siku ya Ijumaa, na sita hawajulikani walipo, wizara ya ulinzi imesema.

Katika taarifa yake, Wizara ya Ulinzi imelaani shambulio dhidi ya kambi ya Garabtisan, kaskazini mwa nchi hii ndogo katika Pembe ya Afrika, na kulishtumu kundi lenye silaha la FRUD (Front for the Restoration of Unity and Democracy), ikilielezea kama "kundi la kigaidi".

Pamoja na kwamba "askari wetu walijhami kishujaa, shambulio hili litakuwa limesababisha vifo vya askari wetu saba, (limewajeruhi wanne na wengine 6 kutoweka", wizara imebainisha na kueleza kuwa utafiti unaendelea ili kuwapata askari waliotoweka na 'kuangamiza' magaidi hawa".

"Genge hili linajulikana sana kwa vitendo vyake vya kutisha na vya uhalifu wa kutisha na kupora watu katika maeneo ya mbali ya nchi," wizara hiyo imesema.

Kundi la FRUD lenye wapiganaji wengi kutoka jamii ya Afar, lilianzisha uasi dhidi ya serikali mwaka 1991, wakidai kutaka kutetea maslahi ya Waafar dhidi ya Issas, jamii nyingine kubwa nchini humo.

Kundi hilo liligawanyika na, ingawa FRUD ni mwanachama wa muungano tawala wa UMP ambao unamuunga mkono Rais Ismaïl Omar Guelleh, tawi lake lenye silaha bado linaendelea na mapambano yake ya kijeshi.

China, ambayo ina maslahi makubwa ya kiuchumi katika Pembe ya Afrika, pia imeweka kambi yake pekee ya kijeshi barani Afrika nchini Djibouti, ambako ina bandari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.