Pata taarifa kuu

Kifo cha mwanasiasa wa upinzani: Equatorial Guinea yalaani azimio la Bunge la Ulaya

Equatorial Guinea imelaanishutumu "kampeni ya propaganda yenye kashfa" ya Bunge la Ulaya baada ya azimio la kulishutumu "kuhusika" kwa kifo cha mpinzani wa kisiasa kizuizini, kulingana na taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP siku ya Jumanne.

Kikao cha Bunge la Umoja wa Ulaya.
Kikao cha Bunge la Umoja wa Ulaya. REUTERS - YVES HERMAN
Matangazo ya kibiashara

Katikati ya mwezi Januari, Vuguvugu la Ukombozi wa Jamhuri ya Tatu ya Equatorial Guinea (MLGE3R), lililohamishwa nchini Uhispania, lilitangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kifo cha mmoja wa wanachama wake, Julio Obama Mefuman, mwenye umri wa miaka 51, raia wa Uhispania , aliyezuiliwa tangu kudaiwa kutekwa nyara mwishoni mwa mwaka 2019 nchini Sudan Kusini.

MLGE3R ilishutumu serikali kwa "kumtesa" Julio Obama Mefuman pamoja na wapinzani wengine watatu waliokamatwa naye mwishoni mwa 2019. Wiki mbili kabla ya hapo, Mahakama ya Uhispania ilifungua uchunguzi kuhusu kutekwa nyara na kuteswa kwa Julio Obama Mefuman, na mpinzani mwingine, pia raia wa Uhispania, Feliciano Efa Mangue.

Utaratibu huu unalenga ndugu watatu wa Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, akiwemo mmoja wa wanawe, Carmelo Ovono Obiang, mkuu wa idara ya upelelezi.

Bunge la Ulaya "linauchulia utawala wa kidikteta wa Guinea ya Ikweta kuhusika" kwa kifo cha Julio Obama Mefuman, na "linalaani vikali ukandamizaji wa kinyama unaofanywa na serikali dhidi ya watetezi wa haki za binadamu", kulingana na azimio la Februari 16.

Wabunge wa Umoja wa Ulaya wametoa wito wa kuachiliwa kwa wanachama wengine watatu wa MLGE3R, kuomba uchunguzi huru kuhusu kifo cha Obama Mefuman, na hali ya wafungwa wa kisiasa.

Katika kujibu, Malabo imeshutumu "kampeni ya propaganda ya yenye kashfa na kuunga mkono vitendo vya kigaidi vilivyoratibiwa na Bunge la Ulaya kwa madhumuni ya kuvuruga usalama wa Equatorial Guinea".

"Equatorial Guinea inakataa kwa uthabiti matamshi yasiyo na msingi ya Bunge la Ulaya kuhusu madai ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo," kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje.

Koloni la zamani la Uhispania, Equatorial Guinea imetawaliwa kwa mkono wa chuma tangu mwaka 1979 na Teodoro Obiang mwenye umri wa miaka 80, ambaye anashikilia rekodi ya dunia ya kuishi maisha marefu madarakani kwa mkuu wa nchi aliye hai, mbali na nchi za kifalme.

“Kuna kelele nyingi (dhidi ya) mradi huu, lakini tunaongeza juhudi za kuhifadhi mazingira”, ameongeza Bw. Makamba, akizungumzia mipango ya upandaji wa miti kwenye njia ya bomba. "Tumezingatia viwango vyote vya mazingira, usalama na haki za binadamu," pia amebainisha.

Mashirika sita yasiyo ya kiserikali yaliishtaki TotalEnergies mbele ya mahakama ya Paris mwishoni mwa 2022, na kulitaka kundi hilo kuheshimu sheria iliyopitishwa mwaka wa 2017 ambayo inalazimisha mashirika ya kimataifa "wajibu wa kuwa makini" kwa shughuli zao duniani. Majadiliano hayo yanatarajiwa tarehe 28 Februari.

Ziwa Albert, mpaka wa asili kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lina wastani wa mapipa bilioni 6.5 ya mafuta yasiyosafishwa, ambayo takriban bilioni 1.4 yanachukuliwa kuwa yanaweza kuokolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.