Pata taarifa kuu

Umoja wa Afrika: Ufunguzi wa mkutano wa 36 mjini Addis Ababa

Nchi 55 zinashiriki tangu Jumamosi, Februari 18, katika mkutano wa 36 wa Umoja wa Afrika, unaofanyika Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. Sherehe za ufunguzi zilifanyika asubuhi katika makao makuu ya umoja huo, mbele ya wakuu wa nchi thelathini na watano na wakuu wanne wa serikali, katika utamaduni safi wa Umoja wa Afrika.

Ufunguzi wa mkutano wa 36 wa wakuu wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 18 Februari 2023.
Ufunguzi wa mkutano wa 36 wa wakuu wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 18 Februari 2023. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mada katika ajenda ni kuharakishwa kwa eneo la biashara huria barani humo, ambalo linatatizika kutekelezwa, pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi na ghasia za kutumia silaha.

Leo asubuhi, Rais wa Comoro, Azali Assoumani, alichukua nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Afrika kutoka kwa Rais wa Senegal Macky Sall kama urais wa zamu wa umoja huo.

"Shirika letu limethibitisha kwa ulimwengu imani yake kwamba nchi zote zina haki sawa," amesema Rais Azali.

Hii ni mara ya kwanza kwa kundi hili la visiwa katika Bahari ya Hindi, ambalo lina wakaazi wasiopungua milioni moja, kuchukua nafasi hii, baada ya vita vikali dhidi ya Kenya, ambayo pia ilikuwa mgombea, hadi Rais William Ruto hivi majuzi alipoamua kujiondoa katika ugombea wake.

Miongoni mwa mambo muhimu ya hotuba yake ya kwanza, Rais wa Comoro aliomba kufutwa kabisa kwa deni la Afrika: "Tunaomba kufutwa kabisa kwa deni la Afrika ili kuwezesha kufufua uchumi wa baada ya janga la Uviko na kuwezesha sisi kukabiliana na athari mbaya za mgogoro wa Ukraine. Mataifa 22 ya Afrika leo, kulingana na Benki ya Dunia, yamo katika hali ya dhiki kuhusiana na deni lao, na kujilimbikizia sehemu kubwa ya dola bilioni 1071 za deni la nje la bara hilo. Kwa uhimilivu wa deni la Afrika, tunahimiza kuanzishwa kwa mfumo wa pamoja wa ulipaji deni ambao utajumuisha zaidi na kuunganisha wadai wa pande mbili na wa kimataifa na pia wadai wa kibinafsi, kwa msaada ulioimarishwa kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa. "

Miongoni mwa changamoto zinazomkabili rais mpya wa Umoja wa Afrika, swali gumu la vikwazo vilivyowekewa Guinea, Burkina Faso na Mali, katika kukabiliana na mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika katika nchi hizi tatu.

Akifungua sherehe hizo, Moussa Faki Mahamat wa Chad, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, alihoji ufanisi wa hatua hii katika kupambana kikamilifu na mabadiliko ya mamlaka kinyume na katiba: "Ni wazi, vikwazo hivi havionekani kuleta matokeo yanayotarajiwa. Kinyume chake, yanazua kutoaminiana kwa mataifa husika na yanaonekana kuwaadhibu watu zaidi na kuwa na athari mbaya kwa uchumi wa nchi husika. Inaonekana kwangu ni muhimu kuangalia upya mifumo ya upinzani dhidi ya mabadiliko yasiyo ya kikatiba ili kuifanya iwe na ufanisi zaidi dhidi ya uovu na kuhusika zaidi na hali ya kiuchumi na kijamii ya raia. Hii bila shaka ni mojawapo ya pembe ambazo mageuzi ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika lazima yazingatie kwa umakini. »

Kuharakisha utekelezaji wa Zlecaf

Moussa Faki, aambaye alikuwa wa kwanza kuzungumza, alikumbusha kaulimbiu ya mwaka huu: kuharakisha uanzishwaji wa Zlecaf, eneo la biashara huria barani Afrika ambalo linatatizika kutekelezwa hadi sasa.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika hakusita kutumia, kama kawaida, lugha ya ukweli, kukashifu "ukosefu wa utashi wa kisiasa" ulioonyeshwa na viongozi wa Afrika, kwa miaka 60, katika utekelezaji wa miradi inayolenga maendeleo na utangamano wa bara, pamoja na matokeo ya "kutopendezwa na raia kuhusiana na" AU.

Hotuba zilifuatiwa, ikiwa ni pamoja na ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ambaye alitoa wito wa kuundwa kwa ujumbe wa amani unaoongozwa na Afrika unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, na ufadhili wa uhakika ili kukabiliana na changamoto za usalama katika bara hilo. ni suala lingine nyeti katika mkutano huu.

Wakati wa hafla hiyo, Antonio Guterres alisema 'ana wasiwasi mkubwa' hasa na hali ya Sahel na mashariki mwa DRC.

Afrika inahitaji hatua kwa ajili ya amani. Umoja wa Mataifa unajivunia kuwa mshirika wa amani barani Afrika, lakini kazi yetu inakuwa ngumu zaidi kila mwaka. Ugaidi na ukosefu wa usalama vinaongezeka na kuna migogoro zaidi. Ninasikitishwa sana na ongezeko la hivi majuzi la ghasia za makundi yenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kusonga mbele kwa makundi ya kigaidi huko Sahel na kwingineko.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.