Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mkutano wa kilele wa AU: Mwanadiplomasia wa Israel afukuzwa katika sherehe za ufunguzi

Kumetokea sintofahamu ya kidiplomasia katika ufunguzi wa mkutano wa 36 wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa baada ya  mwanadiplomasia wa Israel kufukuzwa kwenye sherehe za ufunguzi. Israeli inalaani kitendo 'kibaya'. Umoja wa Afrika, AU, imejibu kwamba mwanadiplomasia husika hakualikwa.

Ufunguzi wa kikao cha 36 cha kawaida cha mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Februari 18, 2023.
Ufunguzi wa kikao cha 36 cha kawaida cha mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Februari 18, 2023. AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Video ya tukio hilo ilisambaa haraka kwenye mitandao ya kijamii. Inaonyesha maafisa wa usalama wa Umoja wa Afrika wakimsindikiza mjumbe kutoka Israel, naibu mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel kwa Afrika, Sharon Bar-li, kutoka nje ya ukumbi wa mkutano.

Ni hatu 'mbaya', kulingana na Israeli. Kwa kujibu, Ebba Kalondo, msemaji wa mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, anaeleza kuwa mwanadiplomasia huyo "aliombwa kuondoka katika eneo hilo" kwa sababu balozi wa Israel katika Umoja w Afrika, Aleli Admasu, ndiye aliyepokea mwaliko wa kibinafsi. "Inasikitisha kwamba mhusika alitumia vibaya nafasi hiyo," msemaji wa mwenyekiti wa Kamisheni ya AU ameongeza.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, hata hivyo, inathibitisha kwa shirika la habari la AFP kwamba Bi. Bar-li alikuwa "amepata kibali kwa njia nzuri na inayostahili", kama "mwangalizi", na inashutumu Umoja wa Afrika kuwa "mateka wa idadi ndogo ya mataifa yenye msimamo mkali kama vile Algeria na Afrika Kusini".

Nyuma ya tukio hili, kuna suala la hadhi ya Israeli, ambalo halijatatuliwa. Mwaka jana, ilizua mijadala mikali, baada ya Moussa Faki kuamua kutoa hadhi ya nchi hii kuwa mwangalizi. Tume iliundwa kuchunguza suala hili nyeti. Lakini haijawahi kukutana.

Vincent Magwenya, msemaji wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, kwa upande wake ameliambia shirika la habari la AFP kando ya mkutano wa Addis Ababa kwamba Israel inapaswa "kuthibitisha shutuma zake".

Kesi hiyo inaonekana vibaya kwa serikali ya Israeli katika uhusiano wake na Afrika

Kwa Israel, hili ni tukio la aibu hasa, wakati ambapo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amefanya kuimarisha uhusiano na bara la Afrika kuwa mojawapo ya malengo makuu ya sera za kigeni za nchi yake.

Suala la hadhi ya waangalizi wa ujumbe wa Israel ndio chanzo cha mfarakano mkubwa ndani ya AU. Katika mkutano wa kilele wa mwaka jana, mjadala kuhusu suala hilo ulisitishwa ili kuepusha kura iliyoonekana kuwa na matatizo.

Mara kadhaa, Mamlaka ya Ndani ya Palestina imewataka viongozi wa Kiafrika kuondoa kibali cha Israel kwa jumuiya hiyo ya bara, ikikashifu utawala wake unaoelezwa kuwa "ubaguzi wa rangi". Juhudi zinaendelea hata hivyo kuruhusu ujumbe wa Israel kushiriki kama mwangalizi katika mijadala hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.