Pata taarifa kuu

Mkutano mdogo wa wakuu wa nchi kuhusu mchakato wa amani mashariki mwa DRC wafanyika Addis

Mkutano mdogo wa wakuu wa nchi kuhusu mchakato wa amani mashariki mwa DRC umefanyika Februari 17, 2023 mjini Addis Ababa, siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika. Suala la kuondolewa kwa uasi wa M23 liligubika mkutano huo.

Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa.
Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa. RFI/David Kalfa
Matangazo ya kibiashara

Mchakato wa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ulikuwa kiini cha mkutano mdogo wa wakuu wa nchi uliofanyika asubuhi ya leo Februari 17, 2023 mjini Addis Ababa, kando ya mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika (AU) unaoanza. siku ya Jumamosi.

Angola na Burundi zimeongoza mkutano huu uliozileta pamoja nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), pamoja na Angola, mpatanishi wa AU kwa (DRC). Walikuwepo marais wa Angola, Burundi, Kongo, Rwanda na rais wa Tanzania. Uganda na Sudan Kusini zote zimewakilishwa na mawaziri wao wa mambo ya nje. Lengo: kuzindua upya mchakato wa Luanda na Nairobi, ambao umesimama.

Majadiliano haya yalichukua zaidi ya masaa manne. Majadiliano "magumu", kulingana na chanzo cha kidiplomasia cha Kenya. "Mazuri na ya kuaminika," kimesema chanzo cha Angola.

Kuondolewa kwa waasi wa M23 kiini cha majadiliano

Hitimisho la mkutano huu mdogo bado halijakamilika, lakini linatarajiwa kutangazwa ifikapo Februari 18. Hata hivyo, inajulikana kwamba suala la kuondolewa kwa waasi wa M23 liligubika majadiliano hayo. Wakuu wa nchi wametaka kuidhinisha ratiba mpya ya kuondoka kwa waasi wa M23 katika maeneo wanayodhibiti - makataa ya hapo awali hayakuzingatiwa - lakini juu ya yote kuamua jinsi ya "kuweka" ratiba hii kwa M23, kinaelezea chanzo cha Kongo.

Kwa upande wa DRC, ilikuwa pia suala la kuwasihi Wakuu wa Nchi kuchukua uamuzi "kulipa jeshi la kikanda (EAC) mamlaka ya kushambulia", ili liende vitani dhidi ya M23 ikiwa kundi hili halitajiondoa na ni wakati jeshi la EAC linazidi kukosolewa nchini DRC kwa uzembe wake.

Katika ufunguzi wa mkutano huo, rais wa Burundi alisikitishwa na ukosefu wa "ufuatiliaji" wa ahadi zilizotolewa katika mikutano ya awali na wakuu wa nchi.

Pia Ijumaa hii, mkutano mwingine unaohusu DRC unatarajiwa kuanza: mkutano wa Baraza la Amani na Usalama. Rais wa Angola, mpatanishi wa AU, atawasilisha ripoti yake.

Kwa upande wa DRC, inasema mikutano hii pia ni fursa ya kusihi Umoja wa Afrika kushiriki zaidi katika utatuzi wa mzozo huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.