Pata taarifa kuu

Sudan inasema 'inakubaliana' na Ethiopia kuhusu bwawa lake kubwa kwenye Mto Nile

Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, mkuu wa Sudan tangu alipofanya mapinduzi, amehakikisha Alhamisi kwamba "amekubaliana katika masuala yote" na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ambaye alimpokea kwa mazungumzo kuhusu bwawa lake kubwa kwenye Mto Nile.

Jenerali Al-Burhane wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Mei 17, 2021.
Jenerali Al-Burhane wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Mei 17, 2021. © REUTERS/Sarah Meyssonnier/Pool/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Bw. Ahmed ambaye anafanya ziara ya kwanza kwa jirani yake tangu mwezi Agosti 2020, amepokelewa na mwenyeji wake Jenerali Burhane, ambaye amehakikisha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba "Sudan na Ethiopia zinakubaliana juu ya pointi zote kuhusu bwawa la Renaissance".

Kwa kuanza ujenzi wa kazi hii kubwa kwenye Mto Blue Nile mwaka 2011, Addis Ababa iliamsha hasira ya Misri, ambayo inahofia usambazaji wake wa maji. Katika miaka ya hivi karibuni, msimamo wa Khartoum umebadilika, wakati mwingine ikiungana na Cairo na nyakati zingine ikiwa pamoja na Ethiopia.

Bw. Abiy hadi sasa hajataja Bwawa Kuu la Renaissance (Gerd) katika jumbe zake za Twitter, na ameendelea kuzungumzia kwa muhtasari kuhusu majadiliano yake mjini Khartoum. Anasema amesisitiza kwa Jenerali Burhane na naibu wake wa pili, Jenerali Mohammed Hamdan Daglo, juu ya 'kanuni ya Ethiopia ya kutoingilia kati'.

Ni muhimu, amesema, "kubeti juu ya uwezo mbalimbali wa watu wa Sudan ili kukabiliana na changamoto zao" na kutafuta "suluhu za ndani" ili kujiondoa katika mgogoro wa baada ya mapinduzi.

Mnamo tarehe 5 Desemba, raia na wanajeshi wa Sudan walitia saini makubaliano ya mfumo wa njia ya kuondokana na mgogoro huo, yakishangiliwa na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na nchi kadhaa, lakini ambayo yanasalia kuwa ya jumla na kuweka makataa machache tu.

Lengo kuu ni kurejesha serikali ya kiraia, kama ilivyoanzishwa baada ya maandamano ya kiraia ambayo yalisababisha jeshi kumuondoa dikteta Omar al-Bashir mnamo 2019.

Majenerali na viongozi wa kiraia waliotimuliwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi walikubali kutia saini lakini makundi ya waasi wa zamani yanakataa makubaliano "ya kipekee". 

Bw Abiy pia alichapisha picha zinazomuonyesha akitabasamu pamoja na viongozi wa Sudan huku uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukidorora mara kwa mara kutokana na masuala mbalimbali.

Tangu 2020, suala la wakimbizi wanaokimbia mzozo huko Tigray lilolimalizika rasmi tangu mwezi Novemba limekuwa suala la msingi. Mara kwa mara, majeshi ya Sudan na Ethiopia yanatuhumiana kila mmoja kwa unyanyasaji na uvamizi.

Ardhi yenye rutuba sana ya kilimo ya Al-Fashaga pia imekuwa mada ya mzozo kwa miongo kadhaa kati ya nchi hizo mbili, lakini wakati mwingine mapigano mabaya yameongezeka huko tangu mwisho wa 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.