Pata taarifa kuu

David Satterfield kuanza ziara ya kikazi kuhusu amani kwenye nchi za pembe ya Afrika

Mjumbe mpya wa Marekani kwenye nchi za pembe ya Afrika, David Satterfield na msaidizi wake State Molly watazuru Saudi Arabia, Sudan na Ethiopia, kuanzia wiki ijayo.

David Satterfield (katikati) alichukua wadhifa wa mjumbe maalum wa Marekani katika Pembe ya Afrika baada ya mtangulizi wake kujiuzulu kutokana na matatizo mawili makubwa.
David Satterfield (katikati) alichukua wadhifa wa mjumbe maalum wa Marekani katika Pembe ya Afrika baada ya mtangulizi wake kujiuzulu kutokana na matatizo mawili makubwa. Adem ALTAN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo itaanzia jijini Riyadh, kisha Khartoum na kumalizia jijini Addis Ababa kati ya Januari 17 mpaka 20.

Akiwa nchini Saudi Arabia, atakutana na kundi la marafiki wa Sudan, ambao wanashirikisha kurejeshwa kwa serikali ya kiraia, baada ya jeshi kuchukua madaraka mwaka uliopita.

Baadaye wataelekea jijini Khartoum, kukutana na wanaharakati ambao wamekiwa akiwandaa maandamano pamoja na viongozi wa jeshi.

Nchini Ethiopia, watakutana na Waziri Mkuu Abiy Ahmed, wakiwa na ujumbe wa kumaliza mzozo wa Tigray ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya mwaka sasa.

Wakiwa Ethiopia watamwambia Waziri Mkuu Ahmed, kusitisha mapigano, kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia mamilioni ya watu wanaoteseka.

Satterfield, aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Uturuki, aliteuliwa katika nafasi hiyo baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mjumbe wa awali Jeffrey Feltman, Januari 6.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.