Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SUDAN-AU

Umoja wa Afrika wahofia wasiwasi wa kutokea kwa mapigano kati ya Sudan na Ethiopia

Tume ya Umoja wa Afrika, umeelezea wasiwasi kuhusu uwezekano wa kushuhudiwa kwa mapigano kati ya kijeshi kati ya Ethiopia na Sudan, na sasa inataka kuwepo kwa mazungumzo.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Fak
Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Fak AP - Ronald Zak
Matangazo ya kibiashara

Wito huu umetolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Moussa Faki Mahamat, baada ya Khartoum kuishtulu Addis Ababa kwa kuwauwa wanajeshi wake saba na raia mmoja, baada ya kutokea kwa makabiliano mpakani wiki iliyopita.

Hata hivyo, Addis Ababa inakanusa kuhusika lakini Sudan inasisitiza kuwa Ethiopia iliwakamata wanajesjhi wake katika êneo la mpaka la Al-Fashaqa, na kuwauwa.

Khartoum siku ya Jumatatu, ilimwagiza Balozi wake aliye jijini Addis Ababa kurejea nyumbani na kusema italiwakilisha kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Nayo Addis Ababa inawashtutumu wanajeshi wa Sudan kuvuka mpaka na kuingia kwenye ardhi yake na kutekeleza mashambulio ambayo yamesababisha majeraha.

Uhusiano wa Khartoum na Addis Ababa umeonekana kuyumba kufuatia mvutano wa matumizi ya maji ya mto Nile, ambao Addis Ababa inatumia kujenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.