Pata taarifa kuu

Ethiopia: UN yatoa wito kusaidi raia waliotoroka makazi yao kufuatia mapigano

Umoja wa Mataifa unaomba msaada wa Dola Milioni 205 kuokoa maisha ya watu zaidi ya Milioni 1 nukta 6 waliokimbia makwao kutokana na mapigano Kaskazini mwa Ethiopia.

Watu waliokimbia makazi yao na wanamgambo kutoka mji wa  Afar wanakaa karibu na shule katika kijiji cha Afdera, Februari 15, 2022.
Watu waliokimbia makazi yao na wanamgambo kutoka mji wa Afar wanakaa karibu na shule katika kijiji cha Afdera, Februari 15, 2022. © EDUARDO SOTERAS/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi,l inasema Dola Milioni 117 zinahitajika kwa haraka kuwasaidia wakimbizi wa Ethiopia na Eritrea, katika majimbo ya Afar, Amhara na Tigray, kupata huduma muhimu za kibinadamu kama chakula na matibabu.

Aidha, kiasi kingine cha Dola Milioni 72 kinahitajika ili kuwasaidia wakimbizi waliokimblia nchini Sudan. 

Mzozo wa miezi 16 Kaskazini mwa Ethiopia, umesababisha watu zaidi ya Milioni Mbili kuyakimbia makwao kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wengi wao wakiwa watoto na wanawake. 

Mbali na changamoto za kibinadamu, vita hivyo, vimesababisha maelfu ya watu, huku watoto zaidi ya Elfu 20 wakishindwa kwenda shuleni. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.