Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Morocco yakusudia 'kutafakari upya' uhusiano wake na Bunge la Ulaya

Wabunge wa Morocco waliamua kwa kauli moja Jumatatu "kutafakari upya" uhusiano na Bunge la Ulaya na kufutilia mbali suala la "uingiliaji kati" katika masuala ndani ya Morocco, kwa kujibu azimio la wabunge wa Umoja wa Ulaya ambao walielezea wasiwasi wao kuhusu uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.

Makao makuu yabunge la Morocco.
Makao makuu yabunge la Morocco. Kafuffle/CC/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Mabaraza mawili ya Bunge yalikutana katika kikao cha mashauriano huko Rabat "kutathmini" azimio la Bunge la Ulaya (EP), ambalo pia lilikuwa na wasiwasi kuhusu madai ya ufisadi yanayoikabili nchi hii.

Katika taarifa iliyochapishwa mwishoni mwa kikao hicho, Bunge la Morocco lilibaini kwamba azimio hili linajumuisha "shambulio lisilokubalika kwa mamlaka, heshima na uhuru wa taasisi za mahakama za nchi hii ya kifalme". "Imeharibu uaminifu kati ya mabunge mawili", imeandikwa katika tamko hili.

Mnamo mwezi Julai, mkuu wa zamani wa jeshi la Israeli Aviv Kochavi alisafiri hadi Morocco, ambayo ilikuwa ziara ya kwanza ya mkuu wa jeshi la Israeli katika nchini Morocco.

Morocco na Umoja wa Ulaya (EU) zimeunganishwa tangu 1996 na makubaliano ya ushirika ambayo yanashughulikia uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kibiashara, hasa katika nyanja ya kilimo na uvuvi.

"Maamuzi (ya wabunge wa Umoja wa Ulaya) hayatatutisha na hatutabadilisha mwelekeo wetu na mbinu zetu", amebaini Mohamed Ghiat, mkuu wa chama cha National Rally of Independents (RNI), chama kikuu cha walio wengi.

"Harufu ya gesi"

Nchi zinazolengwa zaidi ni Ufaransa, inashutumiwa kwa "kuandaa" kampeni dhidi ya Morocco huko Brussels. Bila kusahau Algeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.