Pata taarifa kuu

Sahara Magharibi: Brahim Ghali ateuliwa tena kuwa mkuu wa Polisario Front

Mkutano wa 15 wa Polisario Front, ambao unafanyika kusini mwa Algeria tangu Januari 13 na ambao unatarajiwa kumalizika siku ya Jumapili, umemchaguwa tena, Ijumaa Januari 20, Brahim Ghali kama katibu mkuu wa kundi hilo. Wataalamu kadhaa wanataja kuwepo kwa mgawanyiko wa ndani katika kundi hili la  Polisario.

Brahim Ghali, 73, alichaguliwa tena, Januari 20, 2023, kuwa katibu mkuu wa Polisario Front, wakati wa kongamano lililofunguliwa Januari 13 katika kambi ya wakimbizi ya Dakhla, iliyoko kilomita 170 kusini-mashariki mwa mji wa Tindouf nchini Algeria.
Brahim Ghali, 73, alichaguliwa tena, Januari 20, 2023, kuwa katibu mkuu wa Polisario Front, wakati wa kongamano lililofunguliwa Januari 13 katika kambi ya wakimbizi ya Dakhla, iliyoko kilomita 170 kusini-mashariki mwa mji wa Tindouf nchini Algeria. AFP - RYAD KRAMDI
Matangazo ya kibiashara

Akiwa amehudumu tangu 2016, Brahim Ghali, 73, amedhoofishwa sana na ugonjwa. Ameongezewa muhula mpya wa miaka mitatu na kupata 69% ya kura dhidi ya 31% ya mpinzani wake, Béchir Mustapha. Wajumbe 1,870 wa Polisario walishiriki katika kura hiyo, kulingana na shirika la habari la Sahrawi, SPS.

Uchaguzi ambao haukuwa rahisi sana kwa Brahim Ghali. Kipenzi wa Algiers hakupitisjhwa tena kwa kauli moja. Kongamano la Polisario liliongezwa muda mara mbili kabla ya kuweza kumchagua katibu mkuu wake.

Kwa mujibu wa wachunguzi kadhaa, kundi la Polisario linalotetea uhuru wae liko katika hatua ya mabadiliko katika historia yake, katika mazingira ya mvutano mkali kati ya Algiers na Rabat. Kwa sasa Polisario inakabiliwa na migawanyiko ya ndani ambayo inaidhoofisha.

Kuna, kwa upande mmoja, mkondo unaopendelea vita kama suluhisho pekee la uhuru wa Sahara Magharibi na, kwa upande mwingine, wale wanaopendelea mazungumzo na Moroco, mkondo wa wachache ambao unafanya kazi zaidi ya yote katika kambi za wakimbizi ambao unawatuhumu wasomi wa kisiasa na kijeshi wa Polisario kwa ufisadi na unyanyasaji.

Hata hivyo, Brahim Ghali - ambaye anafurahia kuungwa mkono na Algiers - kwa mara nyingine tena aliwekwa kama mkuu wa Polisario.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.