Pata taarifa kuu

Uhuru wa vyombo vya habari: Bunge la Ulaya laikosoa vikali Morocco

Wabunge wamekosoa vikali kuzorota kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Morocco siku ya Alhamisi, wakisema pia "wamesikitishwa" na madai ya ufisadi yanayoikabili Rabat katika mfumo wa uchunguzi uliofanywa na mahakama ya Ubelgiji na pia kulenga Qatar.

Wabunge wanasisitiza hasa kuhusu kesi ya Omar Radi.
Wabunge wanasisitiza hasa kuhusu kesi ya Omar Radi. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika maandishi yasiyo ya kisheria yaliyopitishwa huko Strasbourg, Bunge la Ulaya "linahimiza" mamlaka ya Morocco "kuheshimu uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari" na mahakama "kuhakikishia waandishi wa habari waliofungwa (. ..) kuwasikiliza na kuchukua uamuzi bila kuegemea".

Wabunge wanasisitiza hasa kuhusu kesi ya Omar Radi. Mwanahabari huyu wa kujitegemea mwenye umri wa miaka 36, ​​anayejulikana kwa misimamo yake dhidi ya utawala, alikamatwa mwaka 2020 na kuhukumiwa mwezi Machi hadi miaka sita jela kwa "ubakaji" na "ujasusi", mashtaka ambayo amekuwa akikanusha kila mara.

"Haki nyingi za upande wa utetezi hazikuheshimiwa, jambo ambalo linatia doa kesi nzima kwa dhuluma na upendeleo", wamebaini wabunge wa Umoja wa Ulaya, ambao wanaomba kuachiliwa kwake kwa muda, na vile vile Taoufik Bouachrine, 54, aliyefungwa tangu 2018, na. Soulaimane Rassouni, 50, mwandishi mwingine wa habari aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani mwaka wa 2022. Wote watatu walipatikana na hatia ya mashtaka kuhusu ubakaji.

Wabunge pia wanataka "kukomeshwa kwa unyanyasaji wa wanahabari wote nchini".

Mamlaka ya Morocco inahakikisha kwamba haki iko huru na kwamba hukumu za waandishi wa habari "hazina uhusiano wowote" na kazi yao ya uandishi wa habari. Shirika la Human Rights Watch, kinyume chake, lilishutumu mwezi Julai maendeleo ya "mbinu za ukandamizaji" dhidi ya wapinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.