Pata taarifa kuu

Sahara Magharibi: Kiongozi wa Polisario Front atishia kuzidisha mapigano dhidi ya Morocco

Chama cha Polisario Front, vuguvugu linalopigania uhuru katika Sahara Magharibi, bado linafanya kongamano lake la 16 katika kambi ya wakimbizi nchini Algeria. Katika kongamano hili la kwanza tangu kuvunjwa kwa makubaliano ya usitishaji mapigano mwaka 2020, Brahim Ghali, katibu mkuu wa vuguvugu hilo linaloungwa mkono na Algeria, ameonekana mkali na kutoa ujumbe wa kuendeleza mapambano ya silaha dhidi ya Morocco. Je, ni ishio la kweli au ni mkakati wa kisiasa?

Brahim Ghali, katibu mkuu wa Polisario Front, mwaka wa 2019.
Brahim Ghali, katibu mkuu wa Polisario Front, mwaka wa 2019. STRINGER / RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mzozo wa Sahara Magharibi unaelezwa na wataalamu kama "uvuguvugu". Mgogoro huu umekuwa na mvutano mdogo tangu kufikiwa kwa makubaliano ya usitishaji mapigano mwaka 1991. Lakini kuanza tena kwa mapigano, mwaka 2020, kumelirudisha swali hilo katika wigo wa kimataifa. Wakati Rabat inang'ang'ania utawala Ufalme wa Morocco katika eneo la  Sahara, Polisario inafutlia mbali "mamlaka ya Morocco katika eneo hilo".

Kwa Morocco iliyojaliwa kuwa na silaha za hali ya juu, Polisario inadai kuwa haina chaguo lingine zaidi ya vita. "Suluhisho pekee" inasema ni kupata uhuru. Kwa hivyo kuna hatari ya kutokea mapigano mapya katika wiki zijazo? Si lazima, anasema Aboubakr Jamai, mwalimu wa mahusiano ya kimataifa huko Aix-en-Provence. Anasema lugha za kivita za Polisario ni mkakati unaolenga kuweka mzozo kwenye rada za jumuiya ya kimataifa na njia ya kutafuta suluhu la kisiasa.

"Kwa maoni yangu, Polisario ina nia ya kutumia lugha za kivita kuwaambia wale ambao wanaweza kushawishi mchakato wa azimio, yaani Umoja wa Mataifa, lakini juu ya yote Marekani na Umoja wa Ulaya, kwamba eneo hilo lina hatari ya kuingia katika sintofahamu na kwamba ni bora kusuluhisha mzozo huu haraka iwezekanavyo na kuutatua kwa kuandaa kura ya maoni kama ilivyoamuliwa na Umoja wa Mataifa muda mrefu uliopita na ambao inarejelea upya mamlaka ya MINURSO [tume ya Umoja wa Mataifa katika Sahara ya Magharibi], na ambao dhamira yake kuu ni kuandaa kura ya maoni. Lugha hii ya vita inakuja juu ya yote kutokana na nia ya Polisario ya kuvutia zaidi uharaka wa kutatua tatizo kwa sababu hali iliyopo inapendelea zaidi Morocco kuliko kitu kingine chochote”.

Tangu 1991, Umoja wa Mataifa umeshindwa kutafuta njia ya kuondokana na mzozo huu. Umoja wa Mataifa unapendekeza uhuru wa eneo hilo kwa miaka mitano, kisha kura ya maoni, lakini vikwazo kwa mpango huu, unaoongozwa na mjumbe maalum wa zamani, Mmarekani James Becker, ni vingi na vinatoka katika kila kambi.

Mara kwa mara, Polisario Front inaangazia kuanza tena kwa mapigano, lakini kwa uaminifu nadhani kwamba hii haiwezekani, Polisario Front pengine ina silaha za kizamani, anaelezea Khadija Mohsen-Finan, mtaalamu wa masuala ya siasa katika Maghreb na ulimwengu wa Kiarabu. Binafsi, ninaamini kwamba njia pekee ya kuondokana na mgogoro huu ni suluhu la kisiasa. Iwapo haiwezi kufanyika kati ya Algeria na Morocco, kuna haja ya kuwepo serikali au kundi la watu wengine wa nje ambao wanaweza kuzirejesha akilini mwa Mataifa haya mawili, ili mzozo wa Sahara Magharibi usiingizwe katika mzozo huu wa kimuundo kati ya Algeria na Morocco.

'Njia pekee ya mzozo huu ni suluhisho la kisiasa'

Tangu 2020, Morocco imeliweka suala la Sahara Magharibi kuwa kipaumbele chake kabisa. Mfalme Mohamed VI ametoa wito kwa nchi washirika "kufafanua" msimamo wao na kumuunga mkono. Kuhusu mchakato wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta suluhu kupitia kura ya maoni, bado unaonekana kuvunjika. "Haikuweza kufanyika kwa sababu wakati mwingine Morocco ilisema hapana, wakati mwingine Algeria ilisema hapana, na kwa kweli Morocco inaogopa sana kura ya maoni ambayo haiwezi kuthibitisha kuwa ni sawa, na Algeria yenye msimamo wa Polisario imejikunja kabisa kwa dhana hii ya kujitegemea. Uamuzi ambao unapendekeza kwamba ingeelekea kwenye uhuru wa Sahara Magharibi. Ni wazi kwamba Umoja wa Mataifa unapitiwa na hatua zinazofanywa na Morocco na Algeria kwa uhuru, lakini pia na Polisario”, kulingana na Khadija Mohsen Finan.

Lakini kinyume chake, Algeria inapata nguvu tena, hasa kwa sababu ya vita vya Ukraine ambavyo vinabadilisha kadi na kuifanya kuwa mchezaji muhimu kwenye uwanja wa kimataifa: "Kuna hitaji la Algeria, kwa kupata nishati, lakini pia msaada katika uwanja wa kimataifa huko Sahel na katika suala la ufikiaji wa Afrika", anahitimisha Khadija Mohsen Finan. Mzozo wa Sahara Magharibi bado ni mzozo mkubwa kati ya Algeria na Morocco.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.