Pata taarifa kuu

Polisi ya Shirikisho la Ethiopia yarejea katika mji mkuu wa Tigray

Polisi ya shirikisho la Ethiopia imeingia tangu siku ya Alhamisi katika mji mkuu wa jimbo lenye matatizo la Tigray, ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 18, "kuhakikisha usalama wa taasisi" ikiwa ni pamoja na viwanja vya ndege, polisi imesema katika taarifa.

Wanajeshi wa serikali ya Ethiopia wakiwa nyuma ya lori kwenye barabara karibu na Agula, kaskazini mwa Mekele, katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia Mei 8, 2021.
Wanajeshi wa serikali ya Ethiopia wakiwa nyuma ya lori kwenye barabara karibu na Agula, kaskazini mwa Mekele, katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia Mei 8, 2021. AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili linakuja karibu miezi miwili baada ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigraya kutia saini makubaliano ya amani mnamo Novemba 2 kumaliza vita vilivyoharibu eneo hili la kaskazini mwa Ethiopia kwa miaka miwili.

"Polisi ya Shirikisho la Ethiopia leo (Alhamisi) imeingia katika mji wa Mekele huko Tigray na kuanza kufanya kazi," ilisema taarifa ya polisi iliyotumwa kwenye mtandao wa Facebook, na kuongeza kuwa watakuwa na jukumu la "kuhakikisha usalama wa taasisi za serikali, ikiwa ni pamoja na viwanja vya ndege, benki na huduma za mawasiliano. .

Kuingia kwa polisi katika mji mkuu wa eneo la kaskazini mwa Ethiopia ni ishara zaidi ya kuhalalisha uhusiano kati ya mamlaka ya shirikisho na eneo la zamani la waasi.

Mekele iliunganishwa kwenye gridi ya taifa ya umeme mnamo Desemba 6. CBE, benki kuu nchini, ilitangaza mnamo Desemba 19 kurejesha shughuli zake katika baadhi ya miji, na mawasiliano ya simu na eneo hilo yameanza kurejeshwa.

Siku ya Jumatano, safari ya kwanza ya ndege ya Ethiopian Airlines katika kipindi cha miezi 18 iliunganisha mji mkuu Addis Ababa na Mekele. Shirika kubwa la ndege barani Afrika limesema limepanga safari za kila siku kuelekea Tigray; itaongeza safari za ndege zake kulingana na mahitaji.

Mapigano hayo yalianza Novemba 2020, wakati Waziri Mkuu Abiy Ahmed alipotuma jeshi kuwakamata viongozi wa Tigray ambao walikuwa wamepinga mamlaka yake kwa miezi kadhaa na ambao aliwashutumu kwa kushambulia kambi za kijeshi za shirikisho.

Idadi ya vifo kamili ya mzozo huu uliosababishwa na unyanyasaji na mauaji, ambao ulifanyika kwa siri, haijulikani. Shirika la International Crisis Group na shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International wameeleza kuwa 'mojawapo ya matukio mabaya zaidi duniani'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.