Pata taarifa kuu
MAKUBALIANO YA AMANI

Ethiopia: Serikali yafanya ziara ya kwanza ya kihistoria Tigray

Ujumbe wa serikali ya Ethiopia umewasili katika mji mkuu wa Tigray siku ya Jumatatu kwa ziara ya kwanza rasmi katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili katika jimbo la waasi, baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani mapema mwezi Novemba.

Marshal Berhanu Jula, Mkuu wa majeshi ya Ethiopia (ENDF), na Jenerali Tadesse Worede, Kamanda Mkuu wa vikosi vya waasi wa Tigray wakibadilishana nakala za makubaliano yao, jijini Nairobi, Novemba 12, 2022.
Marshal Berhanu Jula, Mkuu wa majeshi ya Ethiopia (ENDF), na Jenerali Tadesse Worede, Kamanda Mkuu wa vikosi vya waasi wa Tigray wakibadilishana nakala za makubaliano yao, jijini Nairobi, Novemba 12, 2022. © Brian Inganga / AP
Matangazo ya kibiashara

Kundi hili la maafisa wa ngazi za juu limekwenda Mekele "kusimamia utekelezaji wa mambo makuu ya makubaliano ya amani" yaliyotiwa saini mjini Pretoria, ilmetangaza idara ya mawasiliano ya serikali katika taarifa fupi kwa vyombo vya habari.

Ujumbe huo unajumuisha hasa mshauri wa Waziri Mkuu wa Usalama wa Taifa, Redwan Hussein, mawaziri kadhaa (Haki, Uchukuzi na Mawasiliano, Viwanda, Kazi), Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka inayosimamia miundombinu ya barabara, pamoja na Wakurugenzi Wakuu wa mashirika ya ndege ya Ethiopia na Ethio Telecom, Mesfin Tassew na Frehiwot Tamiru.

Ujumbe huo ulikaribishwa asubuhi na mamlaka hasimu ya kikanda, akiwemo msemaji wake Getachew Reda, kulingana na picha zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Tigray. Serikali ya shirikisho inasema ziara hii "ni dhibitisho kwamba mkataba wa amani uko kwenye njia sahihi na unaendelea".

Serikali na waasi walitia saini kwenye makubaliano ya amani mnamo Novemba 2 huko Pretoria yenye lengo la kumaliza vita ambavyo vimeharibu kaskazini mwa Ethiopia kwa miaka miwili, na kusababisha makumi ya maelfu ya vifo na kulitumbukiza eneo hilo katika janga kubwa la kibinadamu.

Makubaliano haya yanaainisha hasa kupokonywa silaha kwa vikosi vya waasi na kurejeshwa kwa mamlaka ya shirikisho huko Tigray.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.