Pata taarifa kuu

Ethiopia yatishia mashambulizi mapya Tigray kupambana na uhalifu uliopangwa

Nchini Ethiopia, taarifa ya serikali iliyochapishwa Jumamosi Desemba 17 imezua mvutano mpya kati ya mamlaka ya shirikisho na zile za Tigray. Miezi miwili na nusu baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani ya Pretoria, maandishi yaliyochapishwa na shirka la mawasiliano ya umma yanathibitisha kwamba serikali inaweza "kuchukua hatua" kuwalinda wakaazi wa mji mkuu Mekele dhidi ya "uhalifu uliopangwa".

Mji mkuu wa Tigray Mekele ulishambuliwa vikali wakati wa migogoro mikubwa kati ya serikali ya shirikisho ya Ethiopia na vikosi vyaTigray. Hapa, ni baada ya shambulizi la angani, Oktoba 20, 2021.
Mji mkuu wa Tigray Mekele ulishambuliwa vikali wakati wa migogoro mikubwa kati ya serikali ya shirikisho ya Ethiopia na vikosi vyaTigray. Hapa, ni baada ya shambulizi la angani, Oktoba 20, 2021. © AP
Matangazo ya kibiashara

Ni taarifa ya mistari kumi na mbili, iliyochapishwa kwa Kiingereza na Kiamhari, kwenye akaunti ya Twitter ya "idara ya mawasiliano ya Serikali" ya Ethiopia. Haitaji jina la mtu yeyote hasa. Inalaani tu "uhalifu wa kupangwa" unaofanywa "hasa ​​huko Mekele", "wizi" unaofanywa "kwa usaidizi wa silaha" na kulaaniwa kwa serikali kwa simu na "wakazi" wa jiji.

"Wahalifu", ambao hawajatajwa, "watakabiliwa na majukumu yao", inaongeza taarifa kwa vyombo vya habari: "Serikali ya shirikisho itachukua hatua zote muhimu ili kuhakikisha usalama wa watu unalindwa vilivyo".

"Ethiopia inapanga kuzindua upya vita", Rashid Abdi, wa Taasisi ya Utafiti ya Sahan, amepatwa na wasiwasi na kauli hii, akisisitiza kwamba Waziri Mkuu Abiy Ahmed amenufaika kwa umaarufu alioupata wakati wa  safari yake ya upatanisho huko Washington, wakati wa mkutano wa kilele wa Marekani na Afrika.

Mamlaka ya Tigray haikukaa kimya, lakini ilisema kwa uangalifu zaidi. Msemaji wao Kindeya Gebrehiwot amejibu kwa kukumbusha kuwa "uhalifu wa kutisha kama vile ubakaji, mauaji ya kiholela, utekaji nyara na uporaji" unaendelea katika maeneo yanayoshikiliwa na vikosi vya Eritrea na Amhara, ambavyo bado havijajiondoa katika jjimbo la Tigray.

"Nashangaa jinsi watu wanavyowasiliana kwa simu wakati hakuna huduma ya simu huko Mekele," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.