Pata taarifa kuu

Shirika la ndege la Ethiopian Airlines kuanza tena safari kuelekea Tigray

Shirika la ndege la Ethiopian Airlines litarejelea safari za kibiashara kuelekea Tigray siku ya Jumatano baada ya kusitishwa kwa miezi 18 kutokana na mzozo mbaya katika eneo la waasi kaskazini mwa Ethiopia, kampuni hiyo imetangaza siku ya Jumanne Desemba 27.

Shirika la ndege la Ethiopia litaanza tena safari zake kutoka Addis Ababa kwenda Mekele.
Shirika la ndege la Ethiopia litaanza tena safari zake kutoka Addis Ababa kwenda Mekele. © REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linakuja siku moja baada ya ujumbe wa serikali ya Ethiopia kutembelea mji mkuu wa Tigray, Mekele, kwa ziara ya kwanza rasmi katika zaidi ya miaka miwili, na kuashiria hatua kubwa katika mchakato wa amani uliozinduliwa mwezi Novemba.

"Tumefurahishwa kwa dhati na kuanza tena kwa safari zetu za ndege kwenda Mekele," Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo ndege, Mesfin Tasew amesema katika taarifa.

“Kurejeshwa kwa safari hizi za ndege kutaruhusu familia kuungana tena, kutarahisisha kurejeshwa kwa shughuli za kibiashara, Utalii na kuleta fursa nyingine nyingi zitakazohudumia jamii,” ameongeza. Shirika hilo kubwa la ndege barani Afrika limesema limepanga safari za kila siku kuelekea Tigray; litaongeza safari kulingana na mahitaji.

Miongoni mwa wajumbe waliokuwepo siku ya Jumatatu huko Mekele, wakiwemo Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Ethiopia, lakini pia wale wa Ethio Telecom na Benki ya Biashara ya Ethiopia (CBE), washiriki wakuu katika kurejesha huduma za kimsingi ambazo Tigray imezuiliwa kwa mwaka mmoja.

Mekele iliunganishwa kwenye gridi ya taifa ya umeme Desemba 6, CBE, benki kuu ya nchi, ilitangaza Desemba 19 kurejea shughuli katika baadhi ya miji, na mawasiliano ya simu na jimbo hilo yameanza kurejeshwa.

Serikali na waasi wa Tigray walitia saini makubaliano mnamo Novemba 2 kumaliza vita vilivyoharibu kaskazini mwa Ethiopia kwa miaka miwili.

Mapigano hayo yalianza Novemba 2020, wakati Waziri Mkuu Abiy Ahmed alipotuma jeshi kuwakamata viongozi wa Tigray ambao walikuwa wamepinga mamlaka yake kwa miezi kadhaa na ambao aliwashutumu kwa kushambulia kambi za kijeshi za shirikisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.