Pata taarifa kuu

Sudan Kusini kuhamishia shughuli zake za bandari Djibouti

Sudan Kusini inapanga kujenga bandari katika nchi ya Djibouti kama bandari mbadala ya Mombasa, kusafirisha bidhaa kwenda nchi hiyo. 

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akihutubia taifa katika maadhimisho ya miaka 10 ya uhuru, katika Ikulu ya Juba, Sudan Kusini, Julai 9, 2021.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akihutubia taifa katika maadhimisho ya miaka 10 ya uhuru, katika Ikulu ya Juba, Sudan Kusini, Julai 9, 2021. REUTERS - JOK SOLOMUN
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Juba umenunua kipande cha ardhi, ekari tatu  nchini Djibouti,ambapo ujenzi wa bandari mbadala unatazamiwa kuanza hivi karibuni,huu ukiwa mkakati wa nchi hiyo kupunguza utegemezi katika bandari ya Mombasa nchini Kenya. 

Hatua hii inajiri miezi miwili baada ya kitengo cha biashara Sudan Kusini kusema itahamisha bidhaa za nchi yake kwenda bandari ya Djibouti ambayo inasema ni rahisi kwa usafiri kwenda nchi hiyo. 

Mpango huu hata hivyo utakuwa na athari kwa nchi ya Kenya hasa katika bandari ya Mombasa. 

Sudan Kusini imekuwa mteja mkubwa  katika shughuli za bandari ya Mombasa, baada ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,  hii ikimanisha, Kenya inatazamiwa kupoteza kiasi kikubwa cha mapato yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.