Pata taarifa kuu
DJIBOUTI

Djibouti: Ismael Omar Guelleh ashinda uchaguzi kwa 98.58% ya kura

Rais wa Djibouti anayemaliza muda wake Ismaël Omar Guelleh amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo kwa 98.58% ya kura, kulingana na takwimu rasmi za awali.

Rais wa Djibouti Ismael Omar Guelleh amechaguliwa tena kuwa rais, kulingana na matokeo ya awali.
Rais wa Djibouti Ismael Omar Guelleh amechaguliwa tena kuwa rais, kulingana na matokeo ya awali. Eric Feferberg AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Ismael Omar Guelleh amechaguliwa kwa muhula wa tano na wa mwisho na ataiongoza tena nchi hiyo ndogo ya kimkakati ya Pembe la Afrika ambayo ameongoza kwa mkono wa chuma kwa miaka 22.

"IOG", 73, alikuwa akigombea kwa mara ya tano na muhula muhula wa mwisho dhidi ya Zakaria Ismail Farah, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 56 ambaye alikuwa ameingia siasa hivi karibuni na ambaye nafasi yake ya ushindi ilionekana kuwa ndogo.

"Rais Ismael Omar Guelleh amepata kura 167,535, sawa na 98.58% (...) Haya ni matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais uliyofanyika Aprili 9, 2021", Waziri wa Mambo ya Ndani Moumin Ahmed Cheick ametangaza kwenye runinga ya serikali ya RTD karibu saa 9:00 usiku usiku Ijumaa kuamkia leo Jumamosi . Ameongeza kuwa Bwana Farah amepata chini ya kura 5,000. Matokeo ya mwisho, hivi karibuni "yatatolewa na Mahakama ya Katiba".

Mapema jioni ya Ijumaa, Waziri Mkuu Abdoulkader Kamil Mohamed alitangaza kwenye mtandao wa Facebook kwamba "idadi ya wapiga kura itazidi 77%", dhidi ya 68% mnamomwaka  2016. Wapiga kura wengine 215,000 waliojiandikisha (kati ya idadi ya watu 990,000) walitolewa wito kwenda kwa moja ya vituo 529 vya nchi hiyo, ambavyo vingi vilitengwa katika mji mkuu wa Djibouti-ville.

Mnamo mwaka wa 2016, wakati wa uchaguzi wa urais uliopita, Bwana Guelleh alipata karibu 87% ya kura, katika rduru ya kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.