Pata taarifa kuu
VIKWAZO-USALAMA

Washington yamuwekea vikwazo Alpha Condé kwa ukiukaji wa haki za binadamu

Washington siku ya Ijumaa imeweka vikwazodhidi ya rais wa zamani wa Guinea, Alpha Condé, anayeshutumiwa kwa kukandamiza upinzani kwa jeuri kabla ya kupinduliwa katika mapinduzi ya mwaka 2021, kulingana na taarifa ya Wizara ya Fedha ya Marekani.

Alpha Condé alikua rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Guinea, Afrika Magharibi, mnamo 2010, baada ya miongo kadhaa ya tawala za kimabavu au za kidikteta.
Alpha Condé alikua rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Guinea, Afrika Magharibi, mnamo 2010, baada ya miongo kadhaa ya tawala za kimabavu au za kidikteta. AP - Pablo Martinez Monsivais
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo kwa "ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu", vinazuia mali ya mkuu wa zamani wa nchi na kuzuia uhusiano wowote wa kibiashara naye.

Alpha Condé alikua rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Guinea, Afrika Magharibi, mnamo 2010, baada ya miongo kadhaa ya tawala za kimabavu au za kidikteta.

Alikuwa na uhusiano mzuri na Marekani hadi juhudi zake za kurekebisha Katiba mnamo mwezi Machi 2020 ili kuwania muhula wa tatu.

Tamaa yake ya kusalia madarakani ilisababisha kuundwa kwa kundi la wapinzani ambao walipanga, kuanzia Oktoba 2019, maandamano mengi. Walikabiliwa na ukandamizaji mbaya.

Mapema 2020, Condé aliagiza mawaziri wake kuunda kitengo cha polisi kilichojitolea kujibu maandamano ya kumpinga Condé, kwa kutumia vurugu ikiwa ni lazima," Wizara ya Feda ya Marekani imebaini.

Kitengo hiki kilikamata watu kiholela na, karibu na uchaguzi wa urais wa Oktoba 2020, kiliua "zaidi ya watu kumi na wawili wakati hawakuonyesha hatari yoyote", kulingana na taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Bw. Condé, mwenye umri wa miaka 84 leo, alipinduliwa Septemba 5 wakati wa vita vilivyoongozwa na Kanali Mamady Doumbouya, mkuu wa kikosi chake maalum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.